Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema Mwigulu Nchemba ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha kwa lengo la kupanga mkakati wa kuiba fedha kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 205.
Dk Slaa amesema kwamba baraza la jipya mawaziri lililoteuliwa jana, limejaa viraka na halitakuwa na tija kwa Watanzania.
Akizungunza na gazeti moja kwa njia ya simu jana baada ya
kutangazwa kwa baraza hilo, Dk Slaa alitoa maoni yake na kusema kwamba
baraza lililotangazwa kabla ya kufanya kazi tayari limechoka na
halitakuwa na tija kwa Watanzania.
Amesema baada ya kuteua baraza jipya lenye weledi na uzoefu baadhi yao wameteuliwa kwa kubebana.
“Hili baraza halina jipya, halitakuwa na tija kwa Watanzania,
tulikuwa tunahitaji baraza ambalo litawasaidia Watazania katika kupata
matumaini ya maisha yao magumu waliyonayo sas, lakini kinachoonekana
hapa ni viraka vilivyoshonwa tu na si la kuwanufaisha wananchi,”
amesema.
Dk Slaa amesema kwamba uteuzi wa Mwigulu ni kutokana na malengo ya
CCM kujinufaisha wenyewe na kutafuta fedha kwa ajili maandalizi ya
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
“Yaani Baraza la Mawaziri kubwa sana, sasa tulitegemea pia Rais
akifanya mabadiliko apunguze vilevile na baraza, lakini ndiyo kwanza
amewarundika,” amesema.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana amesema
baraza jipya la linaweza kuleta tija hasa katika sekta ya elimu
kutokana na kumweka Mbunge wa Peramiho, Jenister Muhagama. Source:
Tanzania Daima.