Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Waziri Mkuu Msaafu Mzee Cleopa
David Msuya aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jana jijini
Dar es Salaam.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali
Waziri wa nchi Afisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) Bwana Haroun Ali Suleiman aliyelazwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, Jana (Jumanne)
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza
na Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, aliyelazwa katika jengo la Moyo
Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali leo, Jan
15, 2014. Kulia ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal (kushoto) ni Meneja
wa Jengo hilo la Moyo, Sr. Salome Kassanga.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na
Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, aliyelazwa katika jengo la Moyo
Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali leo, Jan
15, 2014. Kushoto ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali
Waziri wa Kazi na Utumishi wa Umma wa Zanzibar, Haruna Ali Suleiman,
aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati
alipofika kumjulia hali leo, Jan 15, 2014. Katikati ni mke wa Makamu,
Mama Zakia Bilal (kushoto) ni Meneja wa Jengo hilo la Moyo, Sr. Salome
Kassanga. Meneja wa Jengo hilo la Moyo, Sr. Salome
Kassanga.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia