Wema ambaye alishindwa kuficha hisia zake na hatimae
kuweka kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa instagram,” …mmmmmh jamani hichi
kitumbo… hakifichiki now…” kuashiria kuwa mabadiliko ya mwili yameshaanza
kuonekana (Picha chini inaonesha ujumbe huo kamili).
Mtandao wa huu ulianza kuhisi taarifa hizo na kuamua
kuzifuatilia kwa karibu ili kujua nini haswa kinaendelea au ni hisia tu. Ndipo
mwandishi alipochukua jukumu la kumtafuta mlimbwende huyo Wema Sepetu na
kugonga mwamba.
Hata hivyo jitihada hizo hazikuishia hapo ndipo kilipopatikana
chanzo cha karibu na Wema na kudai kuwa “ amekuwa akilalamika mabadiliko hayo
na hata kusikika akisema anaihisi ameconsive…” kilisema chanzo hicho bila
kutaka kutambulika hadharani.
“Ni kweli itakuwa hivyo na ndio maana Diamond aliamua
kumtangaza rasmi siku hile ya chrismas” aliongeza.
Diamond ambaye alimtupilia mbali mpenzi wake Penny na
kurudiana na Wema mapenzi yao hayakufichika kwani wakiwa China walipiga picha
za mahaba na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii na kuzua hisia tofauti.
SOMA ZAIDI...
Hivi karibuni wamekuwa karibu sana kimapenzi na kuamua
kuonesha siri zao za ndani bila kuficha, “mwenye macho haambiwi ona… juzi tu
wameweka video zao wakiwa kitandani kila mtu ameziona, lakni pia Diamond
kumnunulia nyumba baada ya kusikia mkataba wake umeisha na kwamba hautoongezwa,
na mambo mengine kibao” kiliongeza chanzo hicho
“lakini tusubiri miezi tisa tu sio mingi na mimba huwahaifichiki bana tutaona tu” alimaliza