Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKATIBU TAWALA WA MIKOA WATANO WATEULIWA UPYA UKU WENGINE WAKIAMISHWA

Makatibu tawala wapya ni ndugu Wamoja A.Dickolangwa anayeenda mkowa wa Iringa ambako alikuwa kaimu katibu tawala wa mkoa. 
Ndugu Abdallah D.Chikota anayeenda Lindi kabla alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Newala, ndugu Symthies E.Pangisa anayeenda mkoa wa Rukwa kabla alikuwa kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mtwara, ndugu Alfred C.Luanda aliyeteuliwa kuwa katibu tawala mkoa wa Mtwara kabla alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora. 
Pia dugu Jackson L.Saitabau anakwenda mkoa wa Njombe kabla alikuwa katibu tawala msaidizi wa mkoa wa Arusha.

Waliohamishwa ni pamoja na Beatha Swai kutoka katibu tawala mkoa wa Pwani kwenda ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI, pia yupo ndugu Sipora J.Liana kutoka mkurugenzi wa jiji la Arusha kwenda ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI na ndugu Benedict ole Kuyan kutoka katibu tawala mkoa wa Tanga kwenda katibu tawala mkoa wa Mara.
Wengine ni ndugu Salum M.Chima kutoka katibu tawala Rukwa kwenda Tanga na Ndugu Mgeni Baruani kutoka katibu tawala mkoa wa Njombe kwenda katibu tawala mkoa wa Pwani.

Wengine ni ndugu Juma R. Idd kutoka mkurugenzi wa jiji la Mbeya na kuwa mkurugenzi wa jiji la Arusha, Eng.Omar Chambo aliyekuwa katibu mkuu wizara ya uchukuzi amehamishiwa mkoa wa Manyara kama katibu tawala wa mkoa na Dkt John Ndunguru aliyekuwa naibu katibu mkuu wa wizara ya ujenzi anahamishiwa mkoa wa Kigoma kama katibu tawala wa mkoa huo.

Post a Comment

0 Comments