Penny ambaye ni mpenzi wa zamani wa Naseeb Abdul "Diamond" haonekani kujutia kitendo cha kumwagana na msanii huyo na badala yake sasa ameanza kuzipa uzito hoja za kumpiga chini Diamond ambaye walidumu naye kimapenzi kwa takribani mwaka mmoja....
Kwa
mujibu wa watu wa karibu na Penny, kitendo cha Diamond
kumpandisha jukwaani Wema Sepetu pale Leaders Club kilipata kila
aina ya laana toka kwa mama mzazi wa Diamond kwani
hakuridhia jambo hilo.....
"Mama
alilalamika sana kuhusu Diamond kumpandisha Wema pale leaders
Club, kimsingi ni kwamba hataki kabisa uhusiano kati ya Diamond
na Wema Sepetu"...Kilisema chanzo kimoja ambacho ni rafiki damu
na familia hiyo.
Wakati
hayo yakijitokeza ndani ya familia ya Diamond, kwa upande wa Wema,
mama yake pia anadaiwa kulalamikia kitendo cha mwanaye kutumika
kila mara kumbusti Diamond pale umaarufu wake unaposhuka...!
"Mama
Wema naye analalamika mwanaye kutumika kama daraja la
kuwavusha watu kwenye umaarufu halafu wakishafanikiwa wanamgeuka
na kumdhalilisha, kifupi ni kwamba hataki kabisa kusikia
mahusiano ya Wema na Diamond" Kilifunguka chanzo hicho.
Aidha
imeelezwa kuwa Diamond amekuwa akimpgia simu Penny mara kwa
mara kumuomba wayamalize lakini Penny amekuwa akimjibu kwa
kifupi kuwa "Nimekuachia Wema Wako"
Taarifa
nyingine toka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kuwa Penny
amekuwa akijisifu kuachana na Diamond kwa hoja kuu tatu:
Moja: Kuondokana na skendo zisizo na faida kwake.
Pili: Kupunguza malalamiko toka kwa familia yake.
Tatu:
Penny aliingia katika mahusiano na Diamond si kwa ajili ya
mapenzi, bali kulipa kisasi kwa Wema ambaye aliwahi kumchukulia
mpenzi wake.
"Hata
kutoa mimba ya Diamond amekuwa akisema kwamba kama angezaa
naye watoto wake wangekuwa na sura mbaya na midomo ya ajabu".Kilimalizia chanzo hicho