JIJI LA ARUSHA YAPITSHA BAJETI YAKE YA SH.BILIONI 37

Halamashauri ya Arusha katika Wilaya ya Arumeru, imepitisha bajeti ya zaidi ya Sh. bilioni 37 zitakazokusanywa na kuelekezwa katika miradi ya maendeleo kwenye vijiji mbalimbali vya halmashauri hiyo.
Kati ya kiasi hicho cha fedha, Sh. 37,319,148,736 zinatarajiwa kupatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani na nje ya halmashauri hiyo.
Akisoma taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Fidelist Lumato, Ofisa Mipango wa Halmashauri, Ersmo Tellun, alisema kuwa bajeti hiyo ni ya mwaka fedha 2014/15.
Wataalam hao waliliambia Baraza la Madiwani kuwa fedha hizo zitapatikana katika mchanganuo wa mapato ya Halmashauri Sh. 2,707,659,500, ruzuku ya fidia ya mapato 431,083,000, ruzuku ya mishahara Sh. 27,255,089,820, ruzuku ya matumizi mengineyo Sh. 2,720,568,000 na miradi ya maendeleo na wafadhili Sh. 4,734,884,416.
Lumato alifafanua kuwa halmashauri hiyo inakisia kutumia Sh. 37,849,293,736 ikiwa ni matumizi ya mishahara, matumizi mengineyo, michango ya Halmashauri katika miradi mbalimbali ya maendeleo, ruzuku ya mishahara, matumizi mengineyo ya ruzuku, miradi ya maendeleo na ruzuku.
Kutokana na ukomo wa bajeti hiyo, Lumato alisema Halmashauri imelazimika kuleta maombi maalum kwa ajili ya miradi ya vijiji 19 ikiwa ni kiasi cha Sh. billioni 5,455,978,106.36.
Miradi mingine iliyoombewa fedha ni mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) Hospitali ya Wilaya ya Oltrumet Sh. bilioni 1.8, ujenzi wa sekondari Sh. milioni 200 na ujenzi wa hostel za sekondari katika maeneo ya wafugaji Sh. milioni 200, Nyingine ni ukamilishaji wa jengo la Halmashauri Sk. milioni 200, ,ujenzi wa vivuko Sh. milioni 800, ujenzi wa bwawa la kukinga maji mafuriko tarafa ya Mukulat na kufanya upembuzi yakinifu wa maeneo.
Baraza hilo lilipitisha bajeti hiyo kwa pamoja na kutaka watendaji kutekeleza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo na kufuatilia mapato ikiwa ni kuwezesha halmashauri hiyo kupata mapato kwa wakati na kutekeleza miradi ya maendeleo.
Halmashauri ya Arusha ni miongoni mwa Halmashauri saba za Mkoa wa Arusha.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post