DINA MARIOS, RUBEN NDEGE, SIYO SIRI TENA, MAMBO HADHARANI




Dina Marios na Ruben Ndege ‘Ncha Kali’.

SIYO siri tena! Uhusiano wa kimapenzi kati ya watangazaji nyota Bongo, Dina Marios na Ruben Ndege ‘Ncha Kali’ sasa upo hadharani.


Kwa muda mrefu Dina na Ruben wamekuwa kwenye uhusiano lakini wamekuwa wakijitahidi kuuficha usijulikane na watu, lakini hata hivyo watu wa karibu hasa wanaofanya nao kazi, walifahamu juu ya uhusiano huo.
Akizungumza katika Kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na Radio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita kwa mara ya kwanza Dina alifunguka kuhusu kuwa na uhusiano na Ruben huku akiweka wazi kuwa ana mimba yake.
“Ni kweli baba mtarajiwa wa mtoto wangu ni Ruben Ndege ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Skylight Band. Wengi hapa kazini mnajua kuwa tulianza naye mbali. Kulikuwa na kupanda na kushuka, mara kwa mara lakini nashukuru sasa uhusiano wetu umeimarika,” alisema Dina.
Alisema, katika muda aliokuwa katika uhusiano na Ruben, kuna wakati walikuwa wakiachana na kurudiana lakini anamshukuru Mungu kwa kuwasimamia na kuwafikisha katika hatua hiyo.
Siku hiyo Dina alikuwa akiaga wasikizaji wake, kwa vile atakuwa na likizo ya uzazi ya miezi minne wakati huu akisubiri kujifungua na kumlea kichanga chake.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post