WADAU,wa uhifadhi wanyama pori kati ya Tanzania na Kenya wameanzisha ushirikiano wa kudhibiti ujangili wa wanyama pori katika mpaka wa kaskazini mwa Tanzania
Ushirikiano
huo unahusisha kubadilishana taarifa za kihalifu,intelijensia na
kufanya doria za pamoja katika mapito ya wanyama pori eneo hilo
ambalo linaunganisha hifadhi za Arusha ,Kilimanjaro na hifadhi ya
Amboseli ya nchini Kenya
Wakizungumza
katika mkutano wa pamoja uliofanyika katika eneo la hifadhi jamii ya
wanyama (WMA) la Enduimet Wilayani Longido, walisema kuwa uwindaji wa
tembo na simba katika eneo la mpaka limekuwa ni tatizo kubwa.
Mkuu
wa usalama katika eneo la hifadhi jamii la enduimet Imanuel Bujiku
alisema kuwa wawindaji wamekuwa wakiwinda wanyama na kukimbilia nchi
jirani kukimbia kukamatwa.
Bujiku
alisema kuwa ushirikiano huo umehusisha idara zote za ulinzi usalama
katika nchi zote zikiwemo polisi na vikosi vya kudhibiti ujangili.
“
Lengo kuu la ushirikiano wetu ni wa kuhakikisha eneo la mapito ya
wanyama kutoka hifadhi ya Amboseli Kenya kuja Tanzania tunaweka ulinzi
wa kutosha kuzuia mauaji ya wanyama “alisema Bujiku
Kuhusu
hali ya ujangili katika eneo la Enduimet alieleza kuwa kuanzia mwezi
januari hadi mwezi octoba mwaka huu jumla ya majangili 16 walikamatwa
pamoja na gari 1 baiskeli 8 pikipiki 5 na watuhumiwa kufikishwa
mahakakani
Naye
mhifadhi jamii kutoka hifadhi ya Amboseli Kenya Francis Irungu alisema
kuwa ushirikiano huo utadhoibiti ujangili na kuleta tija kubwa katka
uhifadhi wanyama pori.
“Hii
ndio mbinu sahihi na endelevu ya kulinda wanyama katika nyakati kama
hizi zenye changamoto kubwa za kihalifu dhiti ya wanyama pori,”alisema
Irungu.
Kwa
upande wake Samwel Ole Kaangi kutoka mfuko wa uhifadhi wa Big life
nchini Kenya alisema kuwa ushirikiano huo umewafanya kuweka mpango kazi
na utekelezaji kutokomeza ujangili katika eneo hilo.
“Wanyama
wanauawa sana katika eneo hili ,tumekubaliana pamoja na uwezo tunao
tutadhibiti ujangili wa tembo na wanyama wengine katika eneo
hili”alisema Ole Kaangi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia