Wafanyakazi wa benki ya Azania tawi la Moshi wakiwa katika picha ya
pamoja wakioneshana upendo siku ya wapendanao.
Keki maalumu iliyoandaliwa na wafanyakazi wa benki ya Azania tawi la
Moshi katika siku ya wapendanao "Valentine Day".
Meneja wa Azania benki tawi la Moshi Hajira Mmambe akiwasha mshumaa
ikiwa ni sehemu ya sherehe ya wapenda nao"Valentine Day'iliyofanyika
katika ofisi za tawi hilo.
Wafanyakazi wa Azania Benki tawi la Moshi wakipena zawadi kama ishara
ya upendo katika siku hiyo ya wapendanao.
Meneja wa tawi hilo Hajra Mmambe(kulia) akifurahia mara baada ya jina
lake kutajwa na mmoja wa wafanyakazi katika benki hiyo kuwa ndiye
ameandaliwa zawadi ya vyombo vya kuhifadhia chakula.
Meneja Mmambe akiweka pozi la picha mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake.
Wafanyakazi wa Azania Benki wakiendelea kupeana zawadi za siku ya
wapendanao"Valentine day".
Ukafika wakati wa kufungua Champagne na kisha wafanyakazi wa Azania
Benki tawi la Moshi pamoja na meneja Hajira Mmambe wakagonga Cheers
kisha wakanywa pamoja.
Wafanyakazi wa benki ya Azania tawi la Moshi wakiwa katika picha ya
pamoja kila mmoja akionesha zawadi aliyopata toka kwa mwenzake ikiwa
ni sehemu ya kumbukumbu katika siku ya wapendanao"Valentine day".
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe akizungumza na
wafanyakazi wa tawi hilo(hawapo pichani)wakati wa hafla fupi ya
sherehe ya siku ya wapendanao iliyofanyika katika ofisi za tawi hilo
mjini Moshi.
Meneja huyo alitoa ujummbe kwa wafanyakazi wa tawi hilo kuendelea
kudumisha upendo na mshikamano katika shughuli za kila siku ili
kukamilisha mhimili mmoja kati ya mihimili mitano ya Azania bank yaani
"Core Values" wa kufanya kazi kama timu"Team spirit"