BREAKING NEWS

Tuesday, February 25, 2014

MILIPUKO MIWILI YATOKEA ZANZIBARI


Mji wa Zanzibar
Polisi Visiwani Zanzibar wamethibitisha kutokea milipuko mitatu ya mabomu kati ya Jumapili na Jumatatu  mchana visiwani humo.
Akizungumza na
mwandishi wetu Erick David Nampesya, mkuu wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame amesema milipuko miwili imetokea leo katika eneo la mgahawa wa Mercury huku mlipuko mwingine ukiwa umetokea katika eneo la Mkunazini, ikifuatia mlipuko uliotokea jana Jumapili katika eneo la Pangawe. Mkuu huyo wa Polisi Zanzibar amesema kuwa hakuna vifo wala majeruhi katika matukio yote matatu wala mali iliyoharibiwa, isipokuwa madhara ya kisaikolojia kutokana na hofu na taharuki kutokana na matukio hayo.
Aidha mkuu huyo wa Polisi ameeleza kuwa upelezi unaendelea ili kuwabaini waliohusika katika matukio hayo ingawa hadi wakati huu hakuna mtu au mshukiwa yeyote aliyekwishamatwa kuhusiana na matukio hayo.
Kuhusu hatua za tahadhari kufuatia matukio hayo Kamanda Makame amesema Polisi wanaendelea kuimarisha ulinzi katika sehemu mbali mbali visiwani humo ikiwa ni pamoja na kufanya doria katika maeneo kadhaa na amewaondoa hofu wananchi wa visiwa hivyo kuhusu usalama wao.
Chanzo:BBC
 Eneo ambalo limeharibika kwa kuchimbika na kitu cha mripoko katika eneo la mkunazini, na kuleta mtafaruku na tukio hilo la mripuko katika majira ya mchana, Katika mripuko huo hakuna mtu aliyepata majarana na uharibifu wa majengo katika eneo hilo.   
 Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Kiongozi wa Kanisa la Mkunazini Ndg. Nuhu Salanya, na Maofsa wa JWTZ , katika eneo la tukio na kutowa maelekezo kwa Uongozi wa Kanisa alipofika katika eneo la tukio kuangalia athari na uharibifu uliotokea katika eneo hilo, wakati wa mripuko huo. 
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Makamanda wa JWTZ waliofika eneo la tukio kuagalia na kuchunguza tukio hilo la mripoko katika eneo la Mkunazini jirani la Kanisani.
Maofisa wa JWTZ wakiangalia eneo la tukio lililochimbika kutokana na kitu kinachodhaniwa ni bomu

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates