Lulu |
Dar es Salaam. Mwigizaji maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael
Kimemeta, amekiri mahakamani kuwa na uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa
mwigizaji mwenzake, Steven Kanumba na pia kuwa ugomvi na Kanumba siku ya tukio
la kifo cha mwigizaji huyo, lakini akakana mashtaka ya kumuua bila kukusudia.
Lulu ambaye yuko nje
kwa dhamana anakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam, akidaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia, kinyume cha Kifungu cha 195 cha
Kanuni za Adhabu (PC), April 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza
Vatican.
Jana Lulu alipandishwa
kizimbani mahakamani hapo na kujibu mashtaka hayo kwa mara ya kwanza tangu
alipofunguliwa kesi hiyo, ambapo alikana kumuua Kanumba bila kukusudia.Kesi
hiyo namba 125 ya mwaka 2012 inasikilizwa na Jaji Rose Teemba.
Kukubali kuwa na uhusiano
wa kimapenzi na Kanumba, ni miongoni mwa mambo manane ambayo mshtakiwa huyo
aliyakiri mahakamani hapo jana, kama mambo yasiyobishaniwa katika kesi hiyo.
Mambo mengine ambayo
Lulu aliyakiri mahakamani hapo yaliyoko katika maelezo ya kesi hiyo ni pamoja
na jina na anuani yake, kwenda nyumbani kwa Kanumba usiku wa tukio hilo, kuwa
na ugomvi na Kanumba pia Kanumba kumzuia kutoka nje ya chumba alipojaribu
kutoka ili akimbie.
Mengine ni kufanikiwa
kutoka nje ya chumba cha Marehemu Kanumba, kumweleza mdogo wa Kanumba (Seth
Bosco) kuwa Kanumba ameanguka, kukamatwa kwake na polisi eneo la Bamaga, saa 11
Alfajiri ya usiku wa tukio hilo na kwamba kweli anashtakiwa kwa kosa la kumuua
Kanumba bila kukusudia.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia