BREAKING NEWS

Monday, February 17, 2014

RANGI AMBAZO MDADA WA LIBENEKE NAZIFAGILIA SAANA NA KIUKWELI NI NZURI ZICHEKI RED NA UJUE MAANA YAKE NYEKUNDU NA PINKI

Enzi hizo ulipokuwa ukivaa nyekundu ilikuwa ukimaanisha kwamba unajitambulisha kwa jamii kwamba wewe ni mtu mwenye msimamo na unayeweza lolote. Pia ilionyesha kama njia ya kuongeza kujiamini kwako iwapo unahudhuria sherehe au tukio la mahojiano iwapo unajihisi kutokuwa na uhakika na ufanyalo.
Na iwapo mwanamke atakuwa amevaa nguo nyekundu ilikuwa ni kielelezo cha kawaida kuwa tayari mwanamke huyo ameshajiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi.

RANGI INGINE NIIPENDAYO NI PINKI

RANGI YA PINK INAMAANISHA: UPENDO NA UZURI.
Rangi  ya Pink ni rangi ya upendo usio na mipaka. Pink ni rangi ya ukimya.  Wapenzi wa Urembo hupendelea rangi ya Pink. Ua  la pink maana yake ni “SINTAKUSAHAU KAMWE “.
NGUVU YA RANGI YA PINK
Pink ni mchanganyiko wa rangi nyekundu na nyeupe.Na kiwango cha nguvu ya pink inategemeana na ni kiasi gani cha wekundu kilichopo. Ingawa nyeupe ni muhimu kwa ajili kukamilisha,huku nyekundu ikisaidia kutimiza umuhimu huo.


Rangi ya PINK hujumisha nguvu hizo. Urembo uliosheheni rangi ya PINK iliyokoza kama rangi ya magenta inaelezea kusawazisha mambo yasiyokaa vema na vurugu.Baadhi ya wafungwa hutumia rangi ya PINK iliyokoza kuondoa tabia za ukatili.
Rangi ya PINK hutumika kuelezea hisa za kujali, upole,kujijali na kupenda sambamba na kukubalika.
KUVAA RANGI YA PINK
Vaa rangi ya  pink iwapo unataka kujiwakilisha mwenyewe kama mtu wa amani ,mpole ambaye hatishiki na chochote.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates