NYUMBA 338 ZA JIJI LA ARUSHA ZABOMOA KILOMBERO NA KALOLENI

Halmashauri aya Jiji la Arusha imevunja nyumba zake338 baada ya kushinda kesi iliyofunguliwa na wapangaji Sangito Sumari na wenzake 216 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha.

Operesheni hiyo inayojulikana kama “Operesheni Mongela”ilianza saa 12 asubuhi jana kwa kuvunja nyumba 56 eneo la Kilombero, nyumba 198 eneo la Kaloleni na nyumba 84 katika eneo la Themi.

Wengi walitegemea kuibuka vurugu wakati wa uvunjaji nyumba lakini hadi mchana hapakuwa na pingamizi kwa wapangaji badala yake wenyewe walihamisha vitu vyao mapema jana asubuhi kabla ya zoezi la kuvunja kuanza.

Hata hivyo kuvunjwa kwa nyumba hizo kumeleta neema kwa baadhi ya watu wakiwamo vijana wanaokusanya vyuma chakavu kuvamia maeneo hayo na kuokota kila aina ya chuma au kitu ambacho waliamini kinaweza kuuzwa na kuwapatia fedha.

Akiwa eneo la Kaloleni baada ya kukamiliza kuvunjwa nyumba za  Kilombero, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mongela alisema, ‘Operesheni Mongela’ ilipata baraka zote za viongozi wa Serikali wanasiasa wakiwamo madiwani wote Mbunge na Meya wa Jiji.


About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia