Maofisa ugani 10 wa Wilaya za Babati na Mbulu, Mkoani
Manyara, wamepatiwa pikipiki zenye thamani ya sh75 milioni, zitakazowasaidia
kutoa huduma kwa jamii inaozunguka msitu wa Nou uliopo kwenye wilaya hizo.
Pikipiki hizo 10 zilitolewa kwa maofisa hao wa Serikali juzi mjini
Babati na shirika la Farm Africa,
kupitia mradi wake wa usimamizi endelevu mfumo wa ikolojia wa msitu wa Nou, kwa
ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Babati Vijiji Zainab Mnubi alisema maofisa
ugani hao watatumia usafiri huo kwa lengo la kufanya kazi na watu 150,000 wa
wilaya hizo wanaoishi kuuzunguka msitu huo.
“Tumieni pikipiki hizo Honda XL, mlizozipata kupitia mradi huo kwa
kuhakikisha msitu unaendelezwa na kutunzwa kwani wanawake na vijana ndiyo
watakuwa waathirika wakubwa wa misitu pindi ukiharibika,” alisema Mnubi.
Naye, Mratibu wa mradi huo, Philipo Mbaga alisema pikipiki hizo zimetolewa
kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wanaoishi kando kando ya msitu wa Nou na
zitalipiwa na mradi huo bima, leseni ya barabarani, matengenezo madogo na
mafuta.
“Mradi
huu wa mwaka 2014-2016 utakapokamilika, pikipiki zitakuwa mali ya wakala wa
msitu nchini (TFS) na halmashauri za wilaya zitawajibika kuhakikisha zinatumika
kwa manufaa ya jamii na zinatunzwa vyema,” alisema Mbaga.
Alisema
Farm Africa, TFS, Halmashauri za wilaya na maofisa wa Serikali katika kata wametia
saini mkataba wa makubaliano kuhusu umiliki wa pikipiki na utendaji kazi kwenye
kata husika kwa manufaa ya wakazi wa maeneo husika.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia