TWASIRA YA MKUTANO WA UFUNGUZI WA KAMPENI ZA UBUNGE JIMBO LA KALENGA
Mtoto
wa Marehemu Mkwawa alikuwa anakanusha taarifa kuhusu Yeye Kuunga Mkono
Chadema,Amesema hawezi kuunga Mkono chama ambacho hakieleweki kuanzia
muundo wake na hata maamuzi yake ndani ya Chama.Yeye ni MwanaCCM damu
damu,na ameapa atafia CCM.
Mh:Mwigulu
Nchemba amesisitiza kuwa Kwa namna Marehemu Mgimwa alivyolitumikia
Jimbo lake na kuiletea Heshima Nchi yetu na Jimbo la Kalenga,kuna kila
sababu ya Kuipa nafasi CCM iendelee kutekeleza Ilani yake ndani ya Jimbo
hilo.Mh:Mgimwa tangu kufariki kwake Vyama vya siasa vimekuwa mstari wa
mbele kumsifia kutokana na Utendaji wake Kuanzia Wizara ya Fedha hadi
Jimboni kwake hasa upande wa Miundombinu,Maendeleo yote yaliyofanyika
ndani ya Jimbo la Kalenga ni Matunda ya sera nzuri za CCM na Ilani ya
CCM ndani ya Jimbo hilo.
Pia
Mwigulu amezungumzia kuhusu Amani na Mshikamano ulipo kwa Wananchi wa
Kalenga ni lazima uendelee kudumishwa,Kitendo cha kukaribisha wapinzani
kwenye jimbo hili ni sawa na kukaribisha Vurugu kwasababu Wapinzani hasa
Chadema katika Taifa hili hawana rekodi nzuri ya kudumisha amani kwenye
maneo wanayoongoza.
Kubwa
zaidi Mh:Mwigulu Nchemba ameendelea kuwaomba Wanakalenga kufanya Kampeni
za Ustaarabu,Kampeni za Amani na Utulivu.Kwa MwanaCCM kufanya Vurugu
sio Jambo jema,bali tutumie Amani tuliyonayo kuwaelimisha hata wenzetu
wa Upinzani kufanya siasa za kistaarabu,Waache michezo ya Kusababisha
Vifo kwa Wananchi wasio na hatia yoyote ile.Siasa safi ni zile za
Kupambanisha Sera na Uwezo wa Kujenga hoja majukwaani.
Hivyo
tar.16/03/2014 Wanakalenga Wote wanajitokeze Kupiga Kura na Kumchagua
Mgombea wa CCM Kijana Godfrey William Mgimwa kwa maendeleo ya Wote
Wanakalenga.
............................. .............................. .............................. ......
WAKATI kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la kalenga Iringa
zikiendelea kuchukua kasi naibu katibu mkuu wa chama cha mapinduzi
(CCM) Taifa Mwigulu Nchemba amepiga kambi kwa muda Kalenga huku
akiibua siri nzito ya Chadema kuanza kununua shahada za wapiga
kura.
Mwigulu alisema kuwa kumekuwepo na mbinu chafu inayofanywa na
Chadema kwa kuanza kununua shahada za kupigia kura kwa wananchi wa
jimbo la Kalenga .
Alisema kuwa Chadema wameanza mbinu hiyo chafu baada ya kubaini
wazi kuwa mgombea wa CCM Godfrey Mgimwa tayari amekwisha shida
katika uchaguzi huo kutokana na imani kubwa ya wana kalenga kwa
CCM.
Hivyo aliwataka wananchi kutodanganyika na pesa zinazotolewa na
Chadema kwa kununua haki yao na badala yake kutunza shahada hizo
ili kuzitumia kupiga kura kama sehemu ya haki yao ya Msingi.
"CCM imefanya mambo mengi katika jimbo la Kalenga kama kuboresha
miundo mbinu na mambo mbali mbali yakiwemo afya , elimu ....jambo
ambalo wananchi bado wana imani kubwa na CCM".
Wakati huo huo Chifu Mkwawa Bw Abdu Mkwawa amekigeuka Chadema
kuwa kimedanganya umma kuwa Chifu Mkwawa anakiunga mkono chama
hicho.
Mkwawa alisema kuwa Dr Slaa amedangaya umma kuwa yeye anaunga mkono Chadema. Amesema
hawezi kuunga Mkono chama ambacho hakieleweki kuanzia muundo wake na
hata maamuzi yake ndani ya Chama.Yeye ni MwanaCCM damu damu,na ameapa
atafia CCM.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia