‘Kupitia Magazeti, website ya Kilimanjaro na vipeperushi
kuanzia kesho February 18 2014 kutaonyeshwa category zote za mwaka huu
za kupigiwa kura na Wananchi, Watanzania watatuma kura zao kupitia simu
ya mkononi kupitia 15440, unapendekeza msanii, kikundi au producer gani
aingie kwenye kipengele’ – Kavishe
‘Kwa hiyo Mwaka huu Watanzania watapiga kura mara mbili
ambapo ya kwanza ni nani aingie kwenye category alafu tutarudi tena
kupiga kura nani awe mshindi wa kwanza, yani mwaka huu ile timu ya watu
100 ya Waandishi, Watangazaji na wadau wa muziki kuchagua nani na nani
aingie kwenye category haitofanya hivyo bali itakutana kuhakikisha tu
kama wimbo uliopendekezwa na Wananchi ni wa mwaka husika, uko sehemu
husika na pia kama umekidhi vigezo vya kuingia KTMA’ – Kavishe
MABADILIKO: Kwa mujibu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA),
mabadiliko yaliyofanywa kwenye tuzo za mwaka huu wa 2014 ni kutokana na
maoni na mapendekezo ya wadau wa tasnia ya muziki kutoa sababu
mbalimbali.
Mwaka huu KTMA itakua na category 36 ambapo category 34 ni za kuchaguliwa na mbili zilizobaki ni zile maalum za kuteuliwa.
Mwaka 2013 kulikua na category 37 ambapo Mwaka huu
imeondolewa moja kutokana na maoni mbalimbali ya wadau wa muziki ambapo
category yenyewe ni Mtayarishaji chipukizi wa mwaka.
Category zilizobadilishwa majina mwaka huu 2014 ni
Mtumbuizaji bora wa kike wa muziki badala ya msanii bora wa kike
ilivyokua mwaka jana, mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki badala ya
msanii bora wa kiume mwaka jana, mwimbaji bora wa kiume Taarab ambayo
mwaka jana ilikua msanii bora wa kiume Taarab.
Mwimbaji bora wa kiume bongofleva badala ya mwaka jana
Msanii bora wa kiume bongofleva, mwimbaji bora kiume band ambayo mwaka
jana ilikua msanii bora wa kiume band, mwimbaji bora wa kike bongofleva
badala ya mwaka jana msanii bora wa kike bongofleva.
Mwimbaji bora wa kike Taarab badala ya mwaka jana msanii
bora wa kike Taarab, mwimbaji bora wa kike band badala ya msanii bora
wa kike band.
BASATA wanasema ‘kwa nini kumekua na mabadiliko haya?
ukiangalia maana halisi ya neno Msanii linasadifu au linaleta maana za
kuingia zaidi ya kitu kimoja, kunaweza kuwepo na msanii wa uchongaji,
msanii wa Uchoraji n.k kwa sababu wanafanya kazi ya sanaa ndio maana
tunatumia majina ya kimuziki kwa sababu huku tuko kwenye muziki’
MENGINE: BASATA wanasema >>> ‘mwaka huu tutakua na video
bora ya muziki ya mwaka badala ya video bora ya wimbo, neno muziki lina
uwanja mpana kuliko wimbo…….. pia tutakua na wimbo bora wa Afropop
badala ya wimbo bora wa bongopop, kutakua na wimbo bora wenye vionjo
vya asili ya kitanzania badala ya wimbo bora wenye vionjo vya asili’
‘Jingine ni Msanii bora chipukizi anaeibukia badala ya
msanii bora anaechipukia…. wapo wasanii wengi sana chipukizi huko
mtaani na miziki yao haijasikika, inawezekana amekaa miaka mingi
akifanya kazi zake lakini akaibuka na ameonekana’ – BASATA
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia