BREAKING NEWS

Tuesday, February 18, 2014

MNYIKA ATINGA MAHAKAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI HII LEO


Mbunge wa chadema John Mnyika  katikati akiwa anaongea na mwanasheria wake  Edson Mbogoro kulia pamoja na msaidizi wake mara baada ya kumaliza kutoa ushaidi katika mahakama ya jumuiya ya Afrika mashariki hii leo
MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amesema kuna hatari Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutumia wingi wake kuendelea kuikomoa kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa kuchagua wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) toka vyama vingine endapo hakutakuwa na tafsiri sahihi ya kifungu cha 50 cha sheria iliyounda Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mnyika alitoa kauli hiyo leo wakati akitoa ushahidi mbele ya jopo la majaji watano wa Mahakama ya Afrika Mashariki (EAJC), wakiongozwa na Jaji Justice Butasi wanaosikiliza shauri namba 6/2012 lililofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Antony Komu kupitia CHADEMA.
Alieleza ni vema kipengele hicho kikapatiwa tafsiri sahihi, ili kuepusha hatari hiyo aliyodai alianza kuishuhudia tangu uchaguzi wa mwaka 2006 wakati huo Chama cha Wananchi (CUF) kikiwa kinaunda kambi rasmi bungeni, lakini mwakilishi wa chombo hicho muhimu hakutokana na chama hicho na likajirudia tena kwenye uchaguzi wa mwaka 2012 wakati CHADEMA ikiunda kambi hiyo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates