Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne Mcintosh, akizungumza na wawakilishi wa kampuni ya CFAO Motors kutoka nchi kadhaa za Afrika katika mpango mkakati wa kubadilishana nao mawazo na uzoefu katika shughuli za biashara na masoko katika ukanda wa Afrika.
Dhumuni la wawakilishi hao wa kampuni wa CFAO Motors ukanda wa Afrika ni kutembelea kampuni hiyo kubwa na ya siku nyingi ya magari hapa duniani na kuangalia aina mpya za bidhaa ambazo zipo sokoni na kupata kujifunza kazi mbalimbali za kijamii ambazo kampuni hiyo ya CFAO Motors inafanya hapa Tanzania.
Wawakilishi hao wa kampuni ya CFAO kutoka nchi za Rwanda, Sudan, Afrika Kusini na nchi zingine wamekuja nchi kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na wamefanikiwa kujifunza shughuli mbalimbali za ufundi na utendaji kazi wa kampuni ya CFAO Tanzania.
Wawakilishi hao wa kampuni ya CFAO Motors ukanda wa Afrika pia walipata fursa ya kuangali akarakana ya kampuni hiyo kwenye maeneo ya Vingunguti na kuona shughuli za ufundi kwa magari yao ambapo wateja ambao wanaharibikiwa na magari wanaweza kupata huduma hiyo kwenye karakana ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors, Charles-Edouard CAMBOURNAC akitoa maelezo kwa wawakilishi wa kampuni ya CFAO Motors kutoka ukanda wa Afrika.
Wawakilishi wa kampuni ya CFAO Motors ukanda wa Afrika wakitembelea eneo linalotoa huduma ya kutengeneza kwa teknolojia ya hali ya juu magari ya wateja wa kampuni hiyo pindi yanapopata hitilafu.
Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors, Wayne Mcintosh (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors, Charles-Edouard CAMBOURNAC, wakati wa Ziara ya kujifunza kutoka wawakilishi wa kampuni kutoka nchi kadhaa za Afrika. Kushoto ni Meneja Masoko wa CFAO Motors, Bi. Tharaia Ahmed.
Wawakilishi wa kampuni ya CFAO Motors wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufika makao makuu ya kampuni hiyo.
Baadhi ya kikundi cha wamasai walioburudisha wawakilishi hao kwa kucheza ngoma za Kimasai.
Baadhi ya Wawakilishi hao wakichukua kumbukumbu za matukio kwenye simu zao wakati kikundi cha Kimasai kilipokuwa kinatoa burudani.
Meneja Masoko wa CFAO Motors, Bi. Tharaia Ahmed akifurahi jambo na mmoja wa wawakilishi hao.