Diwani wa kata ya Buger Bw. Emmanuel Tlaqho akitoa shukrani zake kwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (SACP) Liberatus Sabas mara baada ya
kueleza uanzishaji wa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto katika eneo
hilo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akitoa elimu ya Ulinzi Shirikishi kwa viongozi na wananchi wa Tarafa ya Endabashi iliyopo wilayani Karatu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas katikati akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya wananchi wa Tarafa ya Endabashi mara baada ya kumaliza kutoa elimu ya ulinzi shirikishi kwa wakazi hao
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akitoa elimu ya Ulinzi Shirikishi kwa viongozi na wananchi wa Tarafa ya Endabashi iliyopo wilayani Karatu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas katikati akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya wananchi wa Tarafa ya Endabashi mara baada ya kumaliza kutoa elimu ya ulinzi shirikishi kwa wakazi hao
Wananchi wa Tarafa
ya Endabashi iliyopo wilayani Karatu wamefurahishwa na utaratibu mpya wa jeshi
la Polisi wa kupeleka askari 15 kila Tarafa kwa lengo la kuimarisha ulinzi
katika maeneo yao. Akimshukuru Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, kwa niaba ya
wananchi hao Diwani wa kata ya Buger Bw. Emmanuel Tlaqho, alisema kwamba mbali
na mpango huo pia wamepokea kwa mikono miwili uanzishaji wa Dawati la Jinsia na
Watoto.
Bw. Tlaqho alisema
kwamba Dawati hilo litasadia katika mambo mengi ya kijamii ikiwa ni pamoja na
kutatua migogoro ya ndoa na utelekezwaji wa familia. Alisema pamoja na kuwepo
kwa Dawati hilo pia viongozi wa mtaa wa maeneo hayo wanatakiwa kushirikiana na
Jeshi la Polisi katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuwaasa wanandoa ili waishi kwa amani ndani ya familia
zao pia kutotumikisha watoto pamoja na kutowanyanyasa.
Naye Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus
Sabas akizungumza na viongozi na wananchi wa maeneo ya Tarafa hiyo ambayo ina
jumla ya vijiji 16 na wakazi wapatao 68,339, alisema kwamba mpango huo wa
kupeleka askari 15 kila Tarafa una nia ya kuliweka Jeshi la Polisi karibu na
wananchi ili waweze kushirikiana katika utatuzi wa matatizo ya kiulinzi na
kiusalama kabla hayajafika kwa Mkuu wa Polisi wa wilaya.
Kamanda Sabas
aliongeza kwa kusema kwamba, mbali na askari hao kuimarisha ulinzi katika
maeneo hayo pia watakuwa wanatoa elimu ya Polisi Jamii kwa askari wa vikundi
vya ulinzi shirikishi ili wajue namna ya utendaji wa kazi za ulinzi ikiwa ni
pamoja na ukamataji salama na pia kutoa elimu kwa wananchi kupitia mikutano
mbalimbali ili waweze kujua haki zao na wajibu wao katika suala zima la ulinzi.
Kamanda Sabas
aliwasisitizia wakazi wa Tarafa hiyo wawe wanatumia mbinu za Ulinzi Jirani
katika nyumba zao. Alisema suala la ulinzi ni la kila mmoja na haliihitaji
kusubiri kudra ya M/mungu kwani uwezo wa kuzuia uhalifu upo ndani yao.
Akimalizia kutoa
elimu hiyo kwa wakazi hao, Kamanda Sabas aliwaambia katika suala la ulinzi
itikadi za kisiasa na udini hazina nafasi kwani mhalifu anapovamia eneo lolote
hamuulizi mtu kwamba ni wa Chama gani au Dini gani bali yeye anatekeleza kile alichokikusudia.
Kwa upande wake
mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la John Bula alisema kwamba,
inaonyesha dhahiri kwa sasa jeshi la Polisi limeamua kushirikiana na wananchi
kwani katika maisha yake hayawahi kuongea na Kamanda wa Polisi wa Mkoa ana kwa
ana mbali ya kumuona kwenye runinga au akiwa katika msafara wa Viongozi wa kitaifa
lakini kupitia kikao hicho ameweza kuongea naye.
Bw. Bula alisema
kutokana na hamasa iliyotolewa na Kamanda Sabas yeye kwa kushirikiana na
wananchi wenzake watakuwa bega kwa bega na askari hao waliopo tarafani hapo
ambao wanaongozwa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Robert Majenga.
Mpaka hivi sasa
katika Mkoa wa Arusha tayari Kamanda Sabas amekwisha toa elimu juu ya ulinzi
shirikishi kwa wananchi wa Tarafa
mbalimbali za wilaya nne huku bado akisubiri kumalizia wilaya mbili ambazo ni
Ngorongoro na Longido.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia