Naibu Waziri akihutubia |
Naibu Waziri katika picha ya pamoja na wadau wa Jeshi la Polisi wakiwemo wadhamini wa mkutano huo benki ya NMB. |
Na Mwandishi wetu, Moshi
BENKI ya NMB imetoa kiasi cha shilingi milioni 75, kudhamini
mkutano mkuu wa siku sita wa Maafisa wa
Jeshi la Polisi nchini, ulioanza juzi katika chuo cha taaluma ya Jeshi la
Polisi Moshi (MPA), mkoani Kilimanjaro.
Mkutano huo ambao unajumuisha makamishna, makamanda wa mikoa
ya Tanzania bara na Visiwani pamoja na maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi hilo
kutoka Makao makuu, ulizinguliwa na Naibu waziri wa mambo ya ndani, Pereira Ame
Sirima.
Meneja wa NMB, Kanda ya Kaskazini, Vicky Bishubo (kushoto) akifaruhia jambo na maafisa wenzake wa benki hiyo, Saidi Pharseko, Meneja Mikopo Tawi la Nelson Mandela Moshi,Susan Shuma, meneja wateja binafsi makao makuu na Josephine Kulwa, ambaye ni Meneja mauzo makao makuu. |
Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja wa NMB, kanda ya
Kaskazini, Bi. Vicky Bishubo, alisema udhamini huo unajumuisha usafiri wa mabasi
kwa washiriki wote kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani, pamoja na
maandalizi ya mkutano huo.
Alisema pamoja na hayo, NMB imetoa Kompyuta nne zitakazotumika
katika mpango wa Jeshi kupambana na Uhalifu wa Mitanda, Mikoba, Notebook na kalamu.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia