![]() |
Jaji kiongozi akimkabidhi cheti cha ushiriki, mwakilishi wa Baa ya Makanyaga, Freeman Rogarth, baada ya kumalizika kwa warsha hiyo.(picha na mpiga picha wetu). |
![]() |
Jaji kiongozi akimkabidhi mwakilishi wa Baa ya East Afrika, Beda Paschal cheti cha ushiriki katika hafla ya kufunga mafunzo ya namna ya kuchoma nyama. |
KAMPUNI
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager
jana imetoa mafunzo kwa wachomanyama kutoka Baa mbalimbali za Mkoa wa
Moshi na Arusha ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya
Safari Nyama Choma kwa mwaka 2014 yatakayo fanyika katika viwanja vya
General Tyremachi 15 na viwanja vya CCM mkoa kwa Mkoa wa Kilimanjaro
machi 16
mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari,
Meneja masoko wa TBL, Leia Hermenegild alisema lengo la
kutoa mafunzo ni kutoa elimu kwa wachoma nyama ukizingati auchomaji nyama ni moja sehemu ya kujiingizia kipato katika
Bar.
Leiya alisema
kutokana na hali hiyo wakaona ni vema wakaendesha Semina kwa wachoma
nyama ili waweze kukidhi vigezo vya mahitaji ya Wateja ili waweze
kufurahia Nyama choma kama ilivyo kwa vyakula vingine ili kuendana na
kauli Mbiu ya Bia ya
Safari Lager isemayo“ Safari Lager bila nyama choma haijakamilika.”
Aliongeza kuwa baada
ya mafunzo hayo yaliyo tolewa kwa wachoma nyama wa Baa
ambao walitunukiwa vyeti vya ushiriki
pia kutakuwa na mashindano ya kuchoma nyama ambapo washindi 10
watapatikana kutokana na watakaofuzu vigezo namasharti waliyopewa katika
semina hiyo.
Alisema Fainali za Mashindano zitafanyika Machi15
kwa mkoa wa Arusha na machi 16 kwa mkoa wa kilimanjaro,
Mwaka huu ambapo washindi watapewa zawadi kuanzia mshindi wa kwanza
atakaye jinyakulia Shilingi Milioni moja na Kikombe, mshindi wa pili Lakinane,
Mshindi wa tatu Laki 6,
Mshindi wa nne laki nne na Mshindi wa Tano shilingi laki mbili huku mshindi wa Sita hadi wa Kumi watajinyakulia kifuta jasho
cha shilingi 50,000/= kwa kila mkoa.
Alisema namna ya kuwapata washindi ni kutokana na wateja kupiga kura katika utaratibu utakaobandikwa katika
Baa shiriki ambapo mteja atapiga kura kupitia simu ya mkononi ili kuichagua baa
inayo choma nyama vizuri.
Kwaupande
wake Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Laurence Salvia mbaye pia ni Jaji Mkuu wa
mashindano hayo amesema huwezi kuandaa mashindano bila ya kutoa Elimu,
hivyo TBL wamefikiria jambo la msingi sana lenye manufaa kwa waandaaji
yaani wachoma nyama mpaka kwa watumiani yaani mlaji.
Bwana
Lawrence binfsi aliishukuru TBL kupitia bia ya Safari Lager kufikiria
jambo zuri la kufadhili elimu kwa wachoma nyama jambo ambalo sifaida kwa
wachomanyama tubali hata watumiaji sasa watakula nyama inayostahili.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia