Taarifa za awali zilimtuhumu mmiliki wa nyumba ya wageni moja ambaye pia anajihusisha na biashara za madini (jina tunalo) kwamba alimtoa kafara mhudumu huyo. Ilidaiwa kuwa, kila mwaka mtu mmoja katika biashara zake hupoteza maisha ghafla.
Hata hivyo, mfanyabiashara huyo alipoongea na Uwazi juzikati alikanusha vikali tuhuma hizo na kueleza kuwa yeye ni muumini mzuri wa imani yake.
‘’Hao watu wanapotosha sana, unajua kuna mwaka mwanaume mmoja alikufa ghafla kwenye nyumba yangu ya kulala wageni, alikuja na mpenzi wake ila alimeza Viagra ambazo hata polisi walizikuta mezani.
“Sasa watu wasio na nia njema na mimi tukio hilo wanaliunganisha na hili kwamba nawatoa kafara,” alisema.
Kifo cha Blandina kilitokea ndani ya chumba huku mtu mmoja anayedaiwa kuwa mpenzi wake aliyejulikana kwa jina moja la Timo, mkazi wa eneo hilo akihojiwa na polisi.
Marehemu Blandina ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga, anaelezwa na bosi wake huyo kwamba alikuwa kama mtoto wa familia yake kwa vile alimwamini sana. Alifanya kazi hapo kwa miaka 8 na hakuwa na tatilo la kiafya. Bosi huyo alisema mwili wa marehemu uligundulika baada ya mfanyakazi mwenzake wa kiume kumpigia simu saa 2 asubuhi ambapo simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa ndipo alipoamua kwenda kumgongea katika chumba hicho. Alisema baada ya kufika alishangaa kukuta mlango wa chumba chake uko wazi na alipochungulia alibaini kwamba Blandina alikuwa amefariki dunia. Hata hivyo, polisi baada ya kufika na kuufanyia uchunguzi wa awali mwili huo hawakugundua kuwepo kwa jeraha lolote linaloashiria kuuawa, ingawa mwili huo ulipelekwa kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru. Jeshi la Polisi mkoani Arusha limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia