Mkurugenzi
wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Bw.Philemon
Mollel akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Hai Mh.Novatus Makunga msaada wa
Tani nne za unga wenye thamani ya shilingi Milioni 4.2,baada ya wilaya
yake kupata maafa yaliyotokana na mvu zilizoambatana na upepo mkali na
kusababisha badhii ya watu kukosa nyumba za kuishi
Mkurugenzi
wa kiwanda cha kuzalisha unga Arusha Philemon Mollel akiongea mbele ya
wanakijiji(hawapo pichani)namna alivyoguswa na maafa hayo yaliyopelekea
kutoa msaada huo huku kiwataka wafanyabishara,makampuni,watu binafsi
kujitokeza kuwasaidia waanga wa maafa hao,mbali na msaada huo wa tani
nne za unga pia alitoa shilingi Milioni moja kwaajili ya waanga
Mkuu
wa wilaya ya Hai Mh.Novatus Makunga akiwa na ugeni mzito kutoka kampuni
ya Monaban ofisini kwake,lengo la ugeni huo nikutoa msaada wa chakula
kwa waathirika wa maafa ya mvua
Mkurugenzi
wa Monaban kushoto Philemon Mollel akiongelea namna alivyoguswa na
maafa hayo ambayo yalisababisha baadhi ya watu kukosa makazi ,
Kina mama ambao ndio waathirika wa kubwa wa maafa hayo wakisubiria zoezi la kugawiwa chakula cha msaada
Mtendaji wa kijiji Bi.Trea Ramadhani akitoa shukrani zake za dhati kwa mmiliki wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichipo Arusha
Afisa
Tarafa Masama Bw.Nsajigwa Ndagile akisoma taarifa ya madhara
yaliyotokana na mvua hiyo kuwa ni pamoja na kuezuliwa kwa mapaa ya
nyumba,kubomolewa kwa kuta za nyumba na kuharibiwa kwa mazao hasa
migomba hali iliyosababisha baadhi ya kaya kukosa mahali pa kulala hivyo
kujihifadhi kwa majirani
Wanakijiji wakishuhudia msaada ulioletwa kijijini kwao
Mkuu
wa wilaya Novatus Makunga akimkabidhi msaada uliotolewa na kampuni ya
Monaban ,mtendaji wa kijiji cha kwa sadala Bi.Trea Ramadhani msaada
uliogharimu zaidi ya milioni 4,kushoto kaimu mkurugenzi Bw.Zabdieli
Moshi
Mkuu
wa wilaya ya Hai Mh.Novatus Makunga akitoa shukrani zake za dhati kwa
mmiliki wa kiwanda cha Monaban kwa kuweza kuwaletea chakula cha msaada
na kuwataka makampuni,mashirika na watu binafsi kuiga mfano wa Monaban
kwa kuwasaidia waanga wa maafa yaliyotokana na mvua zilizoambatana na
upepo mkali na kusababisha watu kukosa makazi hivi karibuni ktika wilaya
yake
Mama
ambaye ni muathirika wa maafa hayo akitoa shukurani zake kwa mkurugenzi
wa kampuni ya Monaban kwa kuweza kuwakumbuka kipindi cha shida na kudai
kuwa akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli
Nyumba ya familia ya Bibi Aziza Mohammed baada ya kuezuliwa paa
Bibi
Aziza Mohammed kama anavyooneka katika picha baada ya mvua kusababisha
mafaa makubwa kwake iliyosababisha yeye kuishi chooni na mjuuku wake
Wanakijiji wakiwa wanashusha mifuko ya unga ndani ya gari
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia