JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Stella Mugasha,
amesema vitendo vya rushwa vinaidhalilisha Mahakama na kuwafanya
wananchi kuamini kuwa haki inanunuliwa.
Kutokaana na hali hiyo, Jaji Stella amewataka watumishi wa Mahakama
kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu na kwmaba Mahakama imejizatiti
kuwachukulia hatua za kinidhamu na za kijinai watumishi wanaojihusisha
na vitendo hivyo.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika
katika Mahakama Kuu ya Hakimu Mkazi Arusha, aliwataka watu wenye tabia
ya kufungua mashauri mahakamani kwa nia ya kuwakomoa watu wengine au
kukusudia kupata kibali cha muda ili kujinufaisha, ni kutumia Mahakama
kama kichaka cha maovu cha kutimiza maovu yao, kwani Mahakama
haitaacha kuwachukulia hatua.
Jaji Mfawidhi alisema suala zima la utendaji haki kwa wakati
likitekelezwa kwa ufanisi litawezesha Mahakama nchini kuchangia uwepo
wa amani na utulivu.
Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea mkoani Arusha, Wakili
Modesti Akida, alisema ucheleweshaji wa haki unahatarisha amani, hivyo
ni muhimu kwa Mahakama kujikita katika dhamira yake ya utendaji haki
kwa wakati ili kuepusha migogoro