WATANZANIA wametakiwa kudai haki yao ya kuandaliwa daftari la
kudumu la wapiga kura ili chaguzi zinazofanyika kuanzia sasa ziwe huru
na halali.
Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha jana na mwanaharakati wa Maendeleo,
Lilian Wassira alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara yae
katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Wassira alisema ili chaguzi zinazofanyika kwa haki na uhuru, lazima
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ifumue daftari la zamani kwa kuwatoa
wasio na sifa na kuwaandikisha wenye sifa.
Pamoja na NEC, amewataka wadau na wanaharakati wa masuala ya haki za
binadamu kuwahamasisha Watanzania kuhakikisha wanadai daftari la kupiga
kura lenye maboresho kama haki yao ya msingi ili wakubaliwe kupiga
kura.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia