KAMPUNI
ya Msama Promotions imetangaza utaratibu utakaotumika kupiga kura
kuchagua taratibu za ufanyikaji wa Tamasha la Pasaka la mwaka huu
linalotarajiwa kuanza Aprili 20, mwaka huu.
Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha
hilo, Abihudi Mang’era, zoezi la upigaji kura litahusika kuchagua mikoa,
mgeni rasmi na waimbaji watakaoimba katika tamasha hilo.
Mang’era alisema mwaka huu wametumia utaratibu huo ili kuwapa nafasi
mashabiki wa muziki wa Injili kuchagua mikoa, mgeni rasmi na waimbaji
watakaoshiriki katika tamasha hilo.
Alifafanua kuwa, ili kumchagua mgeni rasmi, unaanza na neno Mgeni
Rasmi, Pasaka, unaacha nafasi, kisha jina la mgeni rasmi kwenda 15327.
“Kumchagua mwimbaji unaandika neno Mwimbaji, Pasaka, unaacha nafasi,
jina la mwimbaji, kisha unatuma kwenda namba 15327, sambamba na
kuchagua mkoa, unaandika neno Mkoa, Pasaka, unaacha nafasi, unautaja na
unatuma kwenda namba 15327,” alisema Mang’era.
Makamu huyo wa mwenyekiti alitoa wito kwa Watanzania kupiga kura kuchagua makundi hayo matatu ili kufanikisha tamasha hilo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia