Raisi wa Chama cha Wanasheria
Tanzania ,Tanganyika Law Society (TLS),Francis Stola amesema kuwa kazi ya Bunge
la Katiba itapimwa na wananchi kupitia kura ya maoni ya Katiba
inayowapa mamlaka ya kuikataa katiba hiyo ama kuikubali endapo
wanaona kuwa maoni yao hayakuzingatiwa.
Licha ya kifungu cha 25 cha sheria
ya mabadiliko kutokufafanua madaraka halisi ya tume hiyo lakini pia
wametakiwa kutengeneza katiba inayotakiwa na Watanzania walio wengi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari
katika Mkutano wa chama hicho ,Stola amesema kuwa kiwango cha madaraka ya Bunge
la Katiba hakijaainishwa wazi na sheria hiyo na hata hivyo katiba
watakayoipendekeza itarudishwa kwa wananchi ambao ndio wana mamlaka
kamili katika kuipigia kura ipitishwe ama isipitishwe.
“Wananchi wakiona maoni yao hayamo
wanaruhusiwa kuikataa ,tunaamini madaraka ya Bunge la Katiba hayataathiri
maoni ya wananchi kwasababu Rasimu ya pili ya Katiba imejengwa na Sauti za
watanzania na maoni yao pia ” Alisema Stola
Kwa upande Jaji Mstaafu Agustino
Ramadhani amesema kuwa Bunge la Katiba lina mipaka haliwezi kubadilisha kila
kitu ni kuinoa tu.
“Msimamo wa tume umeshatolewa na na
Mwenyekiti Jaji Warioba ,maoni yangu ni kwamba Wajumbe Waangalie maslahi ya
Tanzania tunayoitaka wasiangalie misimamo ya vyama” Alisema Warioba
Pia amezungumzia suala la posho ya
Wajumbe wa Bunge la Katiba na kueleza kuwa malipo hayo ya kiasi cha laki tatu
300,000 ni kiasi ambacho ni kikubwa kwa Watanzani walioajiriwa na waliojiajiri
hawaingizi hiyo hela kwa siku hivyo amewataka waone ni heshima kubwa wamepewa
kwa kufanya jambo kwa mustakabali wa taifa na hakuna anyeweza kuwalipa kwa kazi
hiyo.
Naye Raisi wa Shirikisho la
Wanamuziki Tanzania ,Ado Novemba Masongo akizungumzia suala la posho ya wajumbe
wa bunge hilo amesema kuwa suala hilo ni fedheha na wamesikitishwa sana na
jambo hilo kwani walipaswa kugharamiwa na taasisi walizotoka ili kulifanya
jambo hilo kwa uhuru zaidi.
“Inasikitisha sana kuna walimu
mishahara yao haifiki laki 3 kwa mwezi,polisi na wanajeshi lakini wao wanaitaka
kwa siku moja,wameonyesha makucha yao mapema tuko tayari kuandaa maandamano
tukishirikiana na wananchi kupinga suala hili” Alisema Ado
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia