Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna
mara alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Muscat kuanza
Ziara ya kikazi nchini Oman, kushoto ni Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman
Mhe. Dr. Rawiyah Al Busaidi, wa kwanza kulia ni Mheshimiwa Ali Ahmed
Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna
wa pili kutoka kushoto akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Elimu ya
Juu wa Oman Mhe. Dr. Rawiyah Al Busaidi, wa pili kulia , wa kwanza
kushoto ni Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhunawa
tatu kulia akiongoza ujumbe wa Zanzibar katika mazungumzo na Waziri
wa Elimu ya Juu wa Oman Mhe. Dr. Rawiyah Al Busaidi akiongoza ujumbe wa
Oman Kushoto , wa nne kushoto ni Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa
Tanzania nchini Oman.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna
kushoto na Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman Mhe. Dr. Rawiyah Al Busaidi
wakitia saini nyongeza katika mkataba wa ushirikiano wa Elimu ya Juu
baina ya Oman na Zanzibar.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna
kushoto akiwa katika Mazungumzo na Waziri Kazi wa Oman kuhusu
ushirikiano katika sekta ya mafunzo ya amali.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna
kushoto akiwa na Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh kulia , Balozi wa Tanzania
nchini Oman alipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Oman
pichani chini maafisa wa ubalozi na ujumbe wa mheshimiwa waziri
wakifuatilia mazungumzo.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa serikali ya Zanzibar Mheshimiwa Ali
Juma Shamhuna, alifanya ziara ya Kikazi nchini Oman kuanzia tarehe 16
hadi 20 February 2014 kwa Mwaliko wa mwenyeji wake Mheshimiwa Dr.
Rawiyah Al Busaidi, Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman.
Ziara
hii ilikuwa na madhumuni makuu ya kuimarisha uhusiano wa kindungu uliopo
baina ya Oman na Tanzania kupitia sekta ya Elimu na kuimarisha uhusiano
wa karibu na ushirikiano baina ya taasisi za elimu kati ya Tanzania na
Oman.
Katika
ziara hii Mhe. Ali Juma Shamhuna alikutana na kufanya mazungumzo na
Mwenyeji wake Dr. Rawiyah Al Busaidi ambapo pia walitia saini nyongeza
katika Mkataba wa Mashirikiano katika Elimu ya Juu baina ya Zanzibar na
Oman . Mheshimiwa Waziri Shamhuna pia alikutana na Waziri wa Elimu wa
Oman Mheshimiwa Dr. Madihana Ahmed Al Shibaniya na Waziri wa Kazi wa
Oman Mheshimiwa Abdullah Nassor Al Bakri, .
Mbali
na kukutana na viongozi hawa wa Oman, Mheshimiwa Waziri Shamhuna alipata
nafasi kutembelea maeneo kadhaa kujonea shughuli mbalimbali za Taasisi
zinazoshughulika na elimu za Oman, alitembelea makumbusho ya Jeshi la
Oman, Chuo cha Ufundi na Teknolojia, chuo kikuu cha Sultan Qaboos na
Baraza la Taifa la Utafiti.
Katika
maeneo yote aliyotembelea Mheshimiwa Waziri Shamhuna alifurahishwa sana
na shughuli za taasisi za elimu Oman na kuridhika na hatua iliyopigwa
na Oman katika sekta ya Elimu na mafunzo ya Amali. Mheshimiwa Waziri
Shamhuna pia alitembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Oman
kujionea shughuli mbalimbali za Ubalozi na pia kuhudhuria hafla ya
chakula cha Usiku kilichoandaliwa kwa heshima yake nyumbani kwa
Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia