BREAKING NEWS

Friday, February 21, 2014

TANGAZO JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA


Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 18 Februari, 2014
Taarifa kwa Umma: Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa.
Taarifa Na.
201402-03
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 8:30 Mchana
Daraja la Taarifa:
Tahadhari
Kuanzia:
Tarehe
19 Februari, 2014
Mpaka:
Tarehe
21 Februari, 2014
Aina ya Tukio Linalotarajiwa
Vipindi vya mvua kubwa (zaidi ya mm 50 ndani ya saa 24) kwa siku
Kiwango cha uhakika:
Wastani (60%)
Maeneo yanayotarajiwa kuathirika
Kanda ya kati (mikoa ya Singida na Dodoma), nyanda za juu kusini-magharibi (mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe) na maeneo ya kusini (Mikoa ya Ruvuma na Morogoro).
Maelezo:
Hali hii inatokana na kuimarika kwa mfumo wa mgandamizo mdogo wa hewa katika rasi ya Msumbiji. Mfumo huu unatarajiwa kuvuta upepo kutoka misitu ya Congo kupitia maeneo tajwa hapo juu.
Angalizo:
Idara zinazohusika na hali ya tahadhari pamoja na wakazi wa maeneo hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Maelezo ya Ziada
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila itakapobidi.
Imetolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates