Kama
ulikuwa haufahamu, habari kuu katika ulimwengu wa Teknohama kwa siku ya
leo ni Facebook kuinunua Whatsapp kwa bei ya dola bilioni 19. Nunuzi
hilo ni la programu pekee na siyo kampuni ingawa wafanyakazi wa
whatsapp watajiunga na timu ya Facebook moja kwa moja, mission za
whatsapp zitaendelea kubaki kama zilivyo, alieleza Jan Koum ambaye ni muanzilishi wa whatsapp.
Kwa
wasio fahamu, whatsapp ni moja ya programu ya simu za mkononi
inayokuwezesha kutuma ujumbe wa simu kupitia kwenye intaneti badala ya
ujumbe mfupi (sms). Kwa kutumia whatsapp, inamaana utaepuka gharama za
sms huku ikiwa imesheheni matumizi mengine mengi zaidi kama kutuma
picha, sauti uliyojirekodi nk.
Hadi
sasa, whatsapp ina watumiaji hai milioni 450 kila mwezi kutoka nchi
nyingi duniani, huku kukiwa na watumiaji wapya zaidi ya milioni moja
kila siku. Hivyo, ni dhahiri kuwa whatsapp ni programu pendwa na yenye
kutumika.
Whatsapp inaweza kutumika kama njia rahisi zaidi ya mawasiliano kwa watu binafsi na hata makampuni, kwa mfano, sisi Dudumizi tunatumia
whatsapp kama njia ya kuwasiliana na mamia ya wateja wetu walio nje ya
nchi na kutuwezesha kupunguza gharama za mwasiliano.
Ingawa
makampuni mengi ikiwemo Facebook yamekuwa yakitegemea huduma za
matangazo kama njia ya kuingeza kipato, whatsapp ni programu ambayo,
huwezi kuonana na matanagazo na wamejizatiti kuwa ni wataendelea
hivyohivyo bila ya matangazo. Na pia whatsapp ni bure kwa kwa mwaka wa
kwanza na huchaji $1 kwa mwaka kama gharama ya kujiunga kwa miaka
inayofuata. Hivyo kabla ya Facbook kuinunua whatsapp ni dhahiri
walishajipanga kwenye hili, kwani, hili ndilo linaloifanya whatsapp iwe
tofauti.
Akielezea
sababu ya kuinunua whatsapp, mwanzilishi wa Facebook alisema,
wameinunua whatsapp kwa sababu whatsapp ina thamani. Na wao wakiwa kama
wafanya biashara lengo lao kubwa ni kuongeza thamani ya biashara yao
illi waendelee kuwa salama. Hivyo, wanaamini nunuzi la whatsapp litakuwa
na tija na manufaa kwa wote, wanunuzi na walionunuliwa. Hivyo ubora na
misingi ya huduma ya whatsapp utaendelea kuwa juu kama ilivyo sasa.
Lakini,
dili hili la kuinunua whatsapp halikuja ghafla, bali limekuja kwa
kuangalia muelekeo na mabadiliko ya watumiaji wa mtandao. Taarifa
zinaonesha kuwa, asilimia zaidi ya 52% ya watumiaji wa mtandao kwa sasa
ni wale wanaotumia simu. Na pia matumizi ya email kama njia ya
mawasiliano yamezidi kupunguasiku hadi siku. Na siku zinavyozidi kwenda
mbele inamaanisha idadi hii itakua. Pia, kwenye uwanja wa ujasiriamali,
unatakiwa kuishi kwa kuyachunga mazingra na siyo kuomba dua mambo
yasibadilike, hivyo ununuzi huu umekuja ili kuhakikisha Facebook inakuwa
na udhibiti wa mazingira ya watumia intaneti na mtandao.Kitendo cha
Facebook kuinunua whatsapp, kinaiwezesha kujikita zaidi kwenye kundi
kubwa la watumiaji wa intaneti ambao wengi ni vijana.
Kwakuwa
watumiaji wengi wa whatsapp ni wa kwenye simu, na kwakuwa yao ni moja
ya programu zenye mamilioni ya watumiaji, hivyo kuimiliki whatsapp
inamaanisha kumiliki hisa kubwa kwenye soko la watumiaji hao. Na hii
itaiweka Facebook katika hali ya kudhitibi soko. la intaneti na mitandao
jamii. Facebook pia watapata njia wa kuwafikia watumiaji hawa moja kwa
moja kama ilivyokuwa kwa instagram, hivyo hii ni moja nunuzi lenye faida
kwao.
Watu
wengi wamekuwa wakijiuliza, je kitendo za Facebook kuinunua whatsapp
kina faida yoyote kwa kampuni? na nini sisi watumiaji wa whatsapp
tutegemee? Kutokna na sababu nilizozitaja juu (thamani), hivyo ni
yumkini kabisa, Facebook wanaweza kufanya kati ya vifuatavyo.
1. Kuiunganisha whatsapp moja kwa moja na Facebook.
Ikumbukwe
kuwa, whatsapp itaendelea kuwa whatsapp, hivyo usifikiri kwamba kesho
hakutakuwa na whatsapp bali watumiaji wote watapelekwa Facebook, la ,
ila whatsapp itakuwa na ushirikiano wa kiutendaji na Facebook na
kuzifanya ziwe imara zaidi. Ila, ili whatsapp iunganishwe na facebook,
ni dhahiri kuwa whatsapp lazima ifanyiwe maboresho na kuongezewa baadhi
ya matumizi ambayo yataiwezesha kuiunganisha moja kwa moja na Facebook,
isiishie kwenye mawasiliano tu. Kunatakiwa kuongezwe / boreshwa zaidi
zile huduma ya kijamii.
Kwa
mfano, tutegemee kuwa na uwezo wa kutuma visasisho(updates) ambavyo
vitaonekana kwenye Facebook yako. Hii itaipe ya maisha yako hapohapo
kwenye whatsapp. Hii itaipeleka whatsapp kufanana sana na moja ya
mtandao unaofanya kazi zake kama whatsapp unaoitwa Wechat.Huu ni mtandao
uliofanikiwa sana kwa China.
2. Kutafuta / alika marafiki wa facebook kwa kutumia namba za simu na siyo email pekee
Facebook
ilipoanza, ilikuwa inategmea sana email kama njia ya kutafuta marafiki,
ila kadri siku zinavyozidi kwenda, matumizi ya email kama njia ya
mawasiliano ya kawaida yamekuwa yakipungua, hivyo kutegemea email
kunaiweka facebook kwenye kikomo cha kutanuka. Kwakuwa whatsapp inatumia
namba za simu, na kwakuwa facebook imeinunua whatsapp, basi tutegemee
kuwa kutakuwa na uwezo kwa watumiaji wa Facebook kuwaalika watu wajiunge
na facebook kwa njia ya ujumbe wa simu, na hii itaunganishwa vyema kwa
kutumia whatsapp.
3. Kuongezwa huduma zaidi ambazo ni za kulipia.
Kwakuwa
lengo la kuwekeza ni kuongeza kipato.Iwe moja kwa moja au la, ni
dhahiri kuwa facebook watakuja na njia zitakazowawezesha kuongeza kipato
kwa kutumia whatsapp, hivyo kutakuwa na huduma zaidi ambazo si za
lazima, ila kama utazihitaji, basi utatakiwa kulipia kiasi fulani. Hii
ni moja ya njia zinazotumika kipindi unaandaa bando la huduma.
Hivyo,kwa watumiaji wa Facebook na Whatsapp, tutegee mambo mengi zaidi.
Usipitwe na chambuzi/ habari za Teknohama zenye mlengo wa Kitanzania, Jiunge Facebook Fan Page yetu. www.facebook.com/ dudumizi
Mkata Nyoni (ITIL)
Email: mnyoni@dudumizi.com Web: Dudumizi.com
Dudumizi Technologies Limited
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia