CONTAGIOUS KUZINDUA KAMPUNI YAO RASMI
Kundi la muziki la Contagious lenye
maskani yake jijini Arusha limejipanga
kujitanua zaidi kimataifa ambapo safari
hii limejipanga kuanzisha kampuni ya kusimamia kazi zao kikamilifu.
Akihojiwa na gazeti hili kiongozi
mkuu wa kundi hilo,Njara Rasolomanana alisema kuwa katika mojawapo ya mikakati
yao ni kutangaza kazi zao kitaifa na kimataifa.
Alisema kuwa wako katika mkakati wa
kuanzisha kampuni ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia kazi zao kwa ufanisi pamoja na kuwaunganisha na mataifa mbalimbali.
Bila kutaja hadharani jina
la kampuni hiyo alisema kwamba malengo ya kampuni hiyo itakuwa ni pamoja na
kusimamia makundi mengine ya muziki ambayo
ni washirika wao yaliyopo katika nchi za Madagascar na Finland.
Njara,ambaye ni raia wa nchini
Madagascar alisisitiza ya kwamba kwa sasa wanaendelea na kazi ya kuibua vipaji
vya wanamuziki wachanga waliopo ndani ya kundi lao.

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia