SWEDEN YAINGIA USHIRIKIANO NA WILAYA YA HAI
WILAYA YA HAI YAINGIA USHIRIKIANO NA SWEDEN
Ujumbe
wa viongozi kutoka wilaya ya Hai wakiwa na mwnyeji wao ambaye ni
mratibu wa miradi mbalimbali ya maendeleo na pia ni diwani,Stina
Johansson (wa tatu kulia).Wengine kutoka kulia ni Novatus Makunga[mkuu
wa wilaya ya Hai],Clement Kwayu[mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya
Hai]Melkizedeck Humbe[Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Hai] na Ester Mbatiani ambaye ni Afisa mipango mkuu wa halmashauri ya
wilaya ya Hai.
Halmashauri
ya wilaya ya Hai,imeingia mkataba wa miaka minne wa ushirikiano na
Manispaa ya Arvidsjaur nchini Sweden unaolenga katika maeneo ya kiuchumi
na kijamii ukiwemo wa teknolojia ya kisasa ya udhibiti wa takataka
kiuchumi kwa kuziwezesha kutengezwa upya bidhaa kwa ajili ya matumizi.
Mkataba
huo ulitiwa saini wakati wa ziara ya ujumbe wa viongozi wa wilaya ya
Hai uliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya Hiyo, Novatus Makunga hivi karibuni
katika makao Makuu ya Manispaa hiyo nchini Sweden.
Wajumbe
wengine Katika ziara hiyo ya siku tano ambao ndiyo waliosaini mkataba
huo ni pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Clement
Kwayu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Melkizedeck Humbe pamoja
na Afisa Mipango wa Halmashauri Ester Mbatian.
Kufuatia
mkataba huo, Halmashauri ya Wilaya ya Hai itapaswa kuandaa na
kuwasilisha katika Manispaa ya Arvidsjaur miradi mbalimbali inayolenga
katika Nyanja za biashara na viwanda vidogo na vya kati.
Maeneo
mengine ya shirikiano huo ni pamoja na elimu na utoaji wa taarifa,
uboreshaji na usimamizi wa mazingira endelevu pamoja na miradi
inayolenga masuala ya ajira kwa vijana.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Hai mwishoni mwa wiki,Makunga amesema
kadhalika ushirikiano ho unalenga katika kuimarisha shughuli mbalimbali
zinazohusiana na masuala ya sekta ya utalii na utawala bora kuanzia
ngazi ya chini kabisa.
“Kwa
kushirikiana na wenzetu tunaandaa mkakati wa kuimarisha mafunzo kwa
jamii katika masuala ya uchumi na shughuli za maendeleo ya Kijamii na
lengo kubwa zaidi ni kwa kundi la vijana”. Amefafanua Makunga.
Ameeleza
kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden[SIDA] ushirikiano
huo pia utatoa fursa kwa Manispaa ya Arvidsjaur kushirikiana na wilaya
ya Hai katika ujenga uwezo kwa halmashauri juu ya namna ya kupata
taarifa mbalmbali za maendeleo na kiuchumi kutoka maeneo ya vijijini
nakuzifanyia kazi.
Amesema
pia ushirikiano huo umelenga katika kuhakikisha halmashauri ya Hai
inaingia katika mfumo wa kisasa wa namna ya kusimamia ukusanyaji wa
mapato na matumizi ya fedha za maendeleo, kuboresha mawasiliano na wadau
mbalimbali ikiwemo kupitia kituo cha halmashauri hiyo cha redio Boma
FM.
Amesemasa
Manispaa hiyo ya Sweden itasaidia katika ujenzi,uboreshaji na
uendelezaji wa kituo cha mafunzo kwa ajili ya maendeleo ya jamii katika
wilayani Hai pamoja na kusaidia katika kuboresha huduma za afya.
Masuala
mengine yatakayotekelezwa kutokana na mahusiano hayo ni pamoja na
Manispaa ya Arvidsjaur kusaidia katika teknolojia ya urudufishaji wa
taka ambapo unawezesha taka ngumu na taka maji kuweza kutumika tena.
Makunga
amesema kuwa suala la udhibiti wa takataka ni changamoto kubwa katika
mji wa Hai ambao hauna dampo huku kukabiliwa na ongezeko la kasi la watu
wanaopenda kuweka makazi ya kuishi na kuendesha shughuli zao za kazi
Arusha,Moshi,Siha na Simanjiro.
“Kwa
wenzetu taka ni rasilimali, inachambuliwa kuanzia ngazi ya familia na
kupelekwa eneo la kutupa taka, kwa kupangwa kuangalia na aina, na
hutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali vikiwemo vikombe, vijiko, sahani
na umeme pamoja na mafuta ya kulainishia vyuma kutumika
upya,”amefafanua.
Ametaja
mengine ambayo yatatiliwa mkazo kutokana na ushirikiano huo ni pamoja
na Manispaa hiyo kusaidia katika kukuza uchumi na kuimarisha miundo
mbinu ya kiuchumi.
Makunga
ameeleza kuwa manispaa hiyo ambayo inamiliki uwanja wa ndege wa
kimataifa imeonyesha kuvutiwa kusaidia uimarishaji wa uwanja wa
kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) uliopo wilayani Hai kwa kuongeza shughuli
za biashara za Anga pamoja na kuboresha miundo mbinu katika Uwanja huo.
Ujumbe
huo uliweza kupata taarifa juu ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa
na Manispaa hiyo zikiwemo za kuchumi, kijamii pamoja na usimamizi bora
wa ukusanyaji na matumizi ya Mapato.
Kwa
mujibu wa nchi ya Sweden, Mamlaka zote za Serikali za Mitaa zinajulikana
kama Manispaa zinaongozwa kwa sheria ya bunge la nchi hiyo ambapo hivi
sasa kuna Manispaa zipatazo 260 nchini Sweden.
Manispaa
hizi zinawajib wa kusimamia masuala ya elimu kuanzia ngazi ya chekechea
hadi Sekondari pamoja na kujenga na kusimamia vituo vya malezi ya wazee
na wasiojiweza.
Kadhalika
manispaa hizi zinawajibu wa kusimamia vituo vya zimamoto na
uokoaji,kusimamia ujenzi na uendeshaji wa viwanja vya ndege,kusaidia
walemavu pamoja na kuunganisha wajiri na waajiriwa.
Pia
Makunga ameeleza kuwa Manispaa hizi zinajukumu la kusimamia vituo vya
elimu ya ujasirimali kwa vijana na masuala ya Utalii ambapo Sweden kila
siku hupokea watalii zaidiya 500,000 wanaotembelea vivutio mbalimbali
katika Manispaa hizo kutoka nchi za ulaya

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia