Serekali
imesema pamoja na juhudi zinazofanywa nayo bado ufuatilia na ukaguzi unaofanyika
mara kwa mara umebaini kuwa viwango vya utekelezaji wa kazi za matengenezo ya
barabara kiko chini ya matarajio ya ofisi ya waziri mkuu Tamisemi na bodi ya
mfuko wa barabara na wadau wengine.
Huku
halmashauri hazifikii malengo yaliowekwa kwa mwaka hali hii haikubaliki kwani
imekuwa ikirudisha nyuma dhamira ya serekali ya kuwa na barabara zinazopitika
muda wote wa mwaka na kuwawezesha wakulima kuyafikia masoko yote ya mazao.
Akifungua
mkutano wa pili wa wadau wa mfuko wa barabara unaotathmini ya utendaji kwa
mwaka wa fedha 2013-14 waziri wan chi tamisemi Hawa Ghasia alisema kuwa hatua
hiyo ni muhimu ya kupanga mikakati itakayowezesha sekta ya barabara kuboresha
maisha ya watanzania.
Ghasia
alisema kuwa moja ya majukumu yao makubwa ni kuhakikisha miradi yote ya ujenzi
inakidhi viwango,matakwa na azma ya serekali pamoja na washirika wake wa
maendeleo na kuwa watendaji hao na wenyeviti,mameya,watatumia mkutano huo wa
siku 5 kujiwekea malengo na mikakati kwa mwaka wa fedha ujao kufikia malengo
tuliyokusudia.
“Rasilimali
tulizonazo zitumike ipasavyo ili thamani ya fedha iweze kupatikana na kuleta
maendeleo watakaoshindwa kwenda na kasi hii waanze kujiweka pembeni mapema
kwani mikakati tulioweka itazisaidia wakala wa barabara(TANROADS)na mamlaka za
serekali za mtaa kutumia fedha kwa ufanisi uwazi na uwajibikaji”alisema waziri
Ghasia
Waziri
alizitaka Halmashauri zihakikishe zinasimamia kikamilifu taratibu za utoaji wa
zabuni na mikataba iainiwe kwa wakati huku hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa
watendaji wote wanaothibitika kusababisha kazi mbovu na upotevu wa fedha za
mfuko wa barabara.
Kwa upande wake
naibu katibu mkuu ofisi ya waziri mkuuTamisemi
Alphayo Kidata alisema kuwa kumukuwa ongezeko la mtandao wa kilomita za
barabara katika mamlaka za serekali za mitaa kufikia km96,096 huku jmla ya
km56,624.69 ziliingizwa kwenye sheria za baraya mwaka 2007 huku kutokana na
uhaba wa fedha ni km30,000 sawa na31% ndizo hutengenezwa kwa mwaka.
Alphayo
alisema kuwa fedha iliyopangwa kwa mamlaka ya serekali za mitaa kwa
mwaka2012-13 ni b127.6 fedha hizi zilipangwa kwa matengenezo ya km30,402 hadi
kufikia mwishoni mwa robo ya tatu miaka hiyo ni kiasi cha tsh48.29 zilikuwa
zimepelekwa kwenye halmashauri zote kwa ajili ya matengenezo ya barabara huku
kiasi tsh.26.27 sawa na aslimia54 zilikuwazimetmuka kwa matengenezo ya
km11,527.
Alisema kuwa
jumla ya bilion41.87 zilivuka robo ya nne ya mwaka wa fedha kutoka na hali hii
na uchelwaji wa kusaini mikataba ndiko kumefanya halmashauri nyingi kushindwa
kufikia malengo ya wadau wa mfuko wa barabara.
Imeonekana
kuwa ufuatiliaji wa zabuni za serekali imekuwa ndiyo chanzo cha uchelewaji na
kuvuka kwa fedha za miradi hiyo kwa kutaka mikataba kwanza baada ya fedha
kufika huku kumekuwa kukichelewesha miradi ya barabara sehemu mbali mbali humu
nchini na kuleta viwango duni vya barabara hali inayodumaza maendeleo,