MEYA WA JIJI LA ARUSHA ROHO JUU,MBOWE AHOJIWA NA POLISI
Wafuasi
wa Chadema wakiandamana kuelekea katika ofisi za Mkurugenzi wa Jiji la
Arusha kwenda kumpongeza kwa kusimamia vizuri uchaguzi wa Madiwani.
Wafuasi
wa CHADEMA wakishangilia ushindi katika maandamano ya amani ya madiwani
wapya na viongozi kwenda kumpongeza Mkurugenzi wa jiji kwa kusimamia
uchaguzi vizuri.
Mbunge
wa Arusha,Godbless Lema akiwa na madiwani wapya wakiingia katika jengo
la Halmashauri jiji kuwatambulisha kwa Mkurugenzi wa jiji,Sipora Liana\
Kitendo cha Chadema kutetea viti vyake vinne vya udiwani kwenye
uchaguzi mdogo wa juzi, kimetafsiriwa kwamba ni kumfanya Meya wa Jiji la
Arusha, Gaudence Lyimo kukalia kuti kavu. Kwa ushindi wake huo, Chadema
kimefikisha viti 15 kwenye Baraza la Madiwani la Arusha wakati CCM
kimebakiwa kuwa na viti 12 wakati TLP ina viti sita.
Pia Chadema
kina nafasi ya kuongeza kiti zaidi kwani ina nafasi moja ya viti maalum
iliyokuwa ikishikiliwa na Rehema Mohamed aliyetimuliwa mwaka 2011.
Mwenyekiti
wa madiwani wa Chadema, Isaya Doita alisema jana kwamba ushindi wa juzi
ni chachu katika msimamo wa chama chao kutaka uchaguzi wa Meya wa Jiji
la Arusha urudiwe akiamini kuwa alichaguliwa kimizengwe.
Doita
ambaye ni Diwani wa Ngarenaro, alisema wana imani muda si mrefu Jiji la
Arusha sasa litapata Meya ambaye amechaguliwa kwa misingi ya sheria.
Chadema
ilitetea viti vya Kata za Themi, Kimandolu, Kaloleni na Elerai
ilivyovipoteza baada ya kuwafukuza waliokuwa madiwani wake kwa kosa la
kukiuka maagizo ya Kamati Kuu ya chama hicho kuhusu mwafaka wa umeya.
Ushindi
huo unakihakikishia wingi wa wajumbe katika baraza hilo la madiwani
hivyo kuwa na fursa kumwondoa madarakani Meya Lyimo. Doita aliahidi kuwa
chama hicho kitakaa leo kutoa msimamo kuhusu suala hilo la umeya wa
Arusha.
Akizungumzia suala hilo, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Arusha,
Mary Chatanda alisema Chadema kisahau suala la kuchagua meya mpya kwani
uchaguzi wake ulishapita.
Chatanda, ambaye pia anaingia katika
vikao vya Baraza la Madiwani la Arusha kutokana na kuwa Mbunge wa Viti
Maalumu, alisema Chadema kinapaswa kufanya kazi na meya wa sasa.
“Unajua
vikao hivi vinaongozwa kwa kanuni, kwa hiyo wingi wao si hoja ya kumvua
meya au kulazimisha kupitisha mambo yao,” alisema
Mamia wafurika Manispaa
Wabunge
wanne wa Chadema jana waliongoza mamia ya wafuasi wa chama hicho katika
shamrashamra ya kuwasindikiza madiwani wanne kwenda kujitambulisha kwa
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha.
Hata hivyo, furaha yao ilizimwa na polisi baada ya kumuomba Mbunge Arusha Mjini, Godbless Lema kuwatawanya.
Wabunge
wengine walikuwa Mchungaji Israel Natse (Karatu), Joshua Nassari
(Arumeru Mashariki) na Grace Mukya (Viti Maalumu) ambao walitokea ofisi
za Chadema Mkoa wakiwa na wafuasi wa Chadema wakiwamo vijana wa
bodaboda, magari na watembea kwa miguu.
Wakati wabunge hao,
wakiwa katika magari yao, Madiwani wanne wa Chadema, walioshinda,
Mchungaji Rayson Ngowi (Kimandolu) Edmund Kinabo(Themi), Mhandisi
Jeremiah Mpinga (Elerai) na Kessy Lewi (Kaloleni), walikuwa katika gari
la wazi.
Hata hivyo, walipofika katika eneo la Halmashauri
waliwakuta polisi wakiwa wametanda katika eneo hilo na kuwaruhusu
wabunge, madiwani na viongozi pekee kuingia. Agizo la Kamanda wa Polisi
Wilaya ya Arusha (OCD), Gillis Mrotto kuwataka wafuasi hao kutawanyika
halikufanikiwa hadi alipomuomba Lema kuwatawanya wafuasi hao.
Akizungumza
na madiwani hao, Mkurugenzi Jiji, Sipora Liana aliwaahidi ushirikiano:
“Nawapongeza na naomba tushirikiane katika kazi. Mimi kwa kawaida
sipendi ubadhirifu.”
Mbowe ajisalimisha Polisi
Jeshi
la Polisi Makao Makuu limemhoji Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
kwa madai kuwa kauli zake alizozitoa baada ya kikao cha Kamati Kuu ya
chama hicho ni za uchochezi.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa
Kambi ya Upinzani Bungeni alihojiwa kutokana na madai kwamba alisema
polisi ndiyo waliohusika na ulipuaji wa bomu Arusha, waliisaidia CCM
kwenye uchaguzi na kumtuhumu Rais Jakaya Kikwete kuhusika na mauaji ya
Arusha kutokana na kukaa kwake kimya.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia