JAMANI TUNAOMBA UMRI WA RAIS NA SPIKA UPUNGUZWE
Kwa mujibu wa mapendekezo ya Rasimu ya kwanza ya Katiba iliyotolewa na
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji mstaafu Joseph
Warioba, Ibara ya 75 (d) inasema mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa
kushika nafasi ya madaka ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano kama ana umri
usiyopungua miaka Arobaini.
Wapendekeza uwe kuanzia miaka 30 ili vijana nao wapewa nafasi kwa kuwa ndiyo wenye nguvu na uwezo kielimu.
Kibondo. Wajumbe wa Baraza la
Katiba la Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma, wamesema wanataka umri wa
kugombea nafasi ya rais uanzie miaka 30 ili kutoa nafasi kwa vijana
kupata nafasi hiyo.
Pia, wamesema wanataka Ibara ya 75 (d) kifungu
hicho kifutwe au kitamke kwamba sifa moja wapo ya mtu kuchaguliwa
kushika nafasi ya urais itakuwa kuanzia miaka 30.
Kwa mujibu wa mapendekezo ya Rasimu ya kwanza
ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na
Jaji mstaafu Joseph Warioba, Ibara ya 75 (d) inasema mtu atakuwa na sifa
ya kuchaguliwa kushika nafasi ya madaka ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano
kama ana umri usiyopungua miaka Arobaini.
Mapendekezo hayo yanakuja huku ikiwa baadhi ya
wanasiasa wakiwamo Mbunge wa Kigoma Kasikazini, Zitto Kabwe na Mbunge wa
Bumbuli, Januari Makamba waliwahi kupendekeza umri wa mtu kugombea
urais uanzie miaka 30.
Umri wa Rais
Akizungumza katika mkutano wa baraza hilo, Mjumbe
wa Baraza la Katiba la Wilaya hiyo, Ibrahimu Juma alisema anapendekeza
umri wa rais uwe miaka 30 na kuendelea.
Alisema kuweka muda wa miaka 40 ni kuwanyima
fursa watu wenye uwezo wa kushika nafasi ya rais, na kwamba inawanyima
haki ya msingi wananchi kuwa viongozi kwani kuna vijana wengi ambao wana
elimu na uwezo wa kushika nafasi hiyo.
“Kwa mujibu wa mapendekezo ya Rasimu ya Katiba
Ibara ya 75 (d), inataja sifa moja ya mtu kuwa rais ni lazima awe na
umri usiopungua miaka 40 sasa kwa maoni yangu napendekeza kifungu hicho
kibadilishwe na iwe miaka 30,”alisema Juma.
Umri wa Spika wa Bunge
Mjumbe wa Baraza hilo, Moris Sewahana akitoa
mapendekezo kwenye sura ya saba ya mapendekezo ya rasimu ya kwanza ya
Katiba alisema, anapendekeza Katiba ifute umri wa Spika wa Bunge kwani
nafasi hiyo inahitaji busara na siyo umri.
Alisema mapendekezo ya rasimu hiyo ni kwamba
sifa ya mtu kumuwezesha kuwa Spika wa Bunge ni lazima awe na umri wa
miaka 40 ni vyema kifungu hiko kikafutwa, kwa madai ni kiwango cha
elimu kilichotajwa kwenye rasimu inatosha kuwa sifa ya msingi.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia