MGOGORO MISRI WAENDELEA WATU AZIDI KUFA



Maafisa wa Misri na wafanyakazi wa afya  wanasema  dazeni za watu wameuawa katika mzozo  baina ya maafisa wa ulinzi na wafuasi wa rais aliyetimuliwa madarakani Mohammed Morsi lakini wafuasi wa Morsi wanasema idadi hiyo ni kubwa zaidi.

Watoa huduma za afya  katika hospitali moja ya  Cairo wamesema  takriban watu 38 wameuawa katika mapigano.


Katika mji wa Alexandria, taarifa  zinasema  watu saba wameuawa  tangu Ijumaa. Chama cha Morsi cha Muslim Brotherhood kinasema idadi ya waliouawa ni mara mbili ya idadi inayoelezewa na maafisa wa Misri.


Wahudumu katika hospitali hiyo mjini cairo wanasema wamelemewa kutokana na wingi wa majeruhi.


Hospitali hiyo imo katika kijiji cha Nasr kilichoko Cairo ambacho pia ni ngome ya kundi la Brotherhood , kijiji ambacho wafuasi wa Mosri wamepiga kambi kwa wiki tatu sasa.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia