Ticker

6/recent/ticker-posts

ZIMAMOTO KILIMANJARO WAPONGEZWA

 
 Vikosi vya askari mgambo na askari polisi ambao ni wanafunzi wa chuo cha taaluma ya Polisi Moshi wakishuka kutoka mlima Kilimanjaro ambako walikuwa wakifanya shughuli za kuzima moto uliowaka jumapili ya Julai
 Mchakamchaka
 Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akiwasili katika viwanja vya ofisi ya hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro KINAPA kuwapokea na kuzungumza na asakari walioshiriki zoezi la kuzima moto mlima Kilimanjaro.
 Askari walioshiriki zoezi la kuzima moto.
 Kaimu mkurunzi wa hifadhi za taifa Martin Loibook akizungumza wakati wa kuwapokea asakri walioshiriki kuzima moto mlima Kilimanjaro.kushoto kwake ni naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nayarandu na katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Issa Faisal.

Askari shujaa
 Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro Erastus Lufunguro akisoma taarifa mbele ya naibu waziri wa maliasili na utalii,Lazaro Nyarandu.
 Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro Erastus Lufunguro akimkabidhi naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu taarifa kuhusiana na moto uliokuwa ukiwaka mlima Kilimanjaro.
 Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akizungumza na kundi la askari walioshiriki zoezi la kuzima moto mlima Kilimanjaro
 Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akizungumza na kundi la askari walioshiriki zoezi la kuzima moto mlima Kilimanjaro
 Wakuu wa vikosi vilivyoshiriki kuzima moto mlima Kilimanjaro.
 Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akiwapongeza askari walioshiriki kuzima moto Mlima Kilimanjaro.
 Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akizungumza na wafanyakazi wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro.
  Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akizungumza na viongozi wa askari mgambo
 Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akizungumza na viongozi wa askari mgambo ,kushoto kwake ni mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro Erastus Lufunguro.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Moshi 
 SERIKALI imeyashukuru makundi mbalimbali pamoja na viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kufanikisha zoezi la kuzima moto katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro ulioteketeza zaidi ya ekari 40 katika eneo la Amboni . 
 Naibu waziri wa maliasili na utamaduni Lazaro Nyarandu ametoa pongezi hizo leo wakati akiwapokea vikosi vya askari polisi wa chuo cha taaluma ya Polisi cha mjini Moshi pamoja na asakari mgambo walioshiriki zoezi hilo la kuzima moto. 
 Amesema serikali imefurahishwa na moyo wa kujitolea uliofanywa na makundi hayo ya askari pamoja na watu wengine kwani wameonesha moyo wa uzalendo wa kuijenga nchi yao na kwamba ushirikiano huo ndio unaohitajika ili kutokomeza majanga mengine yote yanyo tokea katika taifa. Amesema usalama na ubora na kuwepo kwa uhifadhi wa mlima Kilimanjaro utasaidia uchumi wa nchi pamoja na wapenda milima na mazingira duniani kuona uoto wa asili na theruji ya mlima huo vikiendelea kuwepo.
 Awali akiwasilisha taarifa kuhusu kuzuka kwa moto huo Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro Erastus Lufunguro amesema KINAPA iliweka kambi tano maalum kwa ajili ya kuhudumia waliokuwa wakishiriki zoezi la kuzima moto. 
Amesema moja ya kambi hizo ilikuwa eneo la Marangu kwa ajili ya kuhudumia eneo la Kilema juu ambapo zote kwa pamoja zilikuwa na askari mgambo 128 kutoka wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro sanjari na askari 54 waliopo mafunzoni katika chuo cha polisi CCP.

Post a Comment

0 Comments