TENDWA HAMA CHOHOTE KITAKACHO ANZISHA KAMBI YA MAFUNZO YA KIJESHI TUNAKIFUTA
OFISI ya Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini
imevitaka vyama vya siasa kutii agizo la kutoanzisha kambi za mafunzo ya
kulinda amani maarufu kwa jina la mgambo , huku ikisisitiza kwamba itachukua
hatua za kisheria kwa chama chochote kitakachoiuka , ikiwemo
kukifuta.
Aidha ofisi hiyo imesema kuwa Katiba ya nchi imempa jukumu kila mwananchi kulinda amani na usalama wa nchi, pia kujilinda yeye mwenyewe na mali zake kwa kutoa taarifa katika vyombo vya dola pale anaposikia au kuona mtu anataka kufanya au anafanya uhalifu au amemdhuru mtu.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dares Salaam na ofisi hiyo katika taarifa yake iliyoitoa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Rajab Juma kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa kufutia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutangaza hivi karibuni kinakusudia kuanzisha kambi za mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake nchi nzima.
Alisema suala hilo lilitangazwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na kuandikwa katika vyombo vya habari kabla ya chama hicho, kuwasiliana na taasisi husika ikiwemo ofisi hiyo ili kupata ushauri kuwa

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia