CHAMA cha demokrasia na maendeleo chadema
kimesema kuwa kitatumia gamarama ya aina oyote
kulinda kura za uchaguzi mdogo wa
udiwani unaotarajiwa kufanika mapema july 14 mwaka huu katika kata nne za
jijini la Arusha .
Haya yamebainishwa na mbunge wa jimbo la Arusha
mjini Godbless Lema wakati akiongea nagomaa moto waandishi wa habari kuhusiana na uchaguzi wa
udiwani unaotarajiwa kufanyika mapema jul 14 mwaka huu katika kata nne ambazo
ni kalole ,Themi,Kimandolu pamoja na
Elerai.
Alisema kuwa katika kipindi hichi cha uchaguzi
wabunge wapatao 16 watakuwepo kwa ajili kuimarisha ulinzi wa kura pamoja na
vijana wa chadema ikiwa ni pamoja na vikosi maalumu wakiwemo redbrigedi,QX1
hakuna matata na FB6 ngoma moto .
Aidha lema alisema nguvu kubwa zaidi
wanatarajiakuweka haswa maeneo ambayo walikuwa wanapata wasiwasi wa kuibiwa
kura zao ambapo alisema kuwa wamejipanga kuchukua kata zote kwa asilimia zaidi
ya 80% ambapo alibainisha kuwa kimandolu kwa asilimia 92%,kaloleni 82% na Elerai asilimia 82 %.
Wakati huo huo mbunge wa jimbo la Arumeru
mashariki Joshua Nassari ambaye ameingia
jijini hapa kutokea katika hospitali ya muhimbili kwa matibabu alisema kuwa
ingawa amepigwa maeneo mbalimbali mwilini mwaka katika maeneo ya sehemu za
shingo ,kwenye mbavu ,mgongo pamoja na
kifua lakini anashukuru mungu amepona na amerudi rasmi akiwa na afya bora na
kusema kuwa upo tayari kuendelea na mapambano.
"napenda kuwaamba wananchi wangu wa jimbo la
Arumeru mashariki kuwa nimerudi kwa nguvu kubwa na tutaendeleza mapambano pale
tulipoishia na pia nawaambia dhambi
kubwa kuliko yote duniani ni woga"alisema nassari
Aidha alilishutumu jeshi la polisi vikali kwa kwa
kutumia nguvu kubwa kuzuia mapokezi yake
pamoja na kufanya mkutano wa kuongea na wananchi wake katika jimbo lake kwa
kigezo kwamba kuna uchaguzi jumapili wa udiwani wa jiji Arusha
"mimi nawashangaa wanatumia nguvu kubwa
kuzuaia mkutano badala ya kulinda ualifu na tembo wanaoibiwa kila siku katika
hifadhi zetu pamoja na ujambazi wa ungaltd kwa kigezo kwamba kunauchaguzi
katika jiji la arusha wakati mimi nafanyia arumeru katika jimbo
langu............. kunamusiano gani kati ya arumeru na arusha?".alisema
Nassari
Naye mgombea udiwani wa kata ya Elerai
Eng.Jeremia Mpinga akikanusha vikali tuhuma za kujiondoa kwenye kinyanganiro
cha udiwani wa kata yake alisema kuwa ajajiondoa kugombea kata hiyo ya elerai kama baadhi ya mitandao
ya kijamii na watu wanavyodai .
Alisema kuwa uvumi huo umetokea baada ya mbunge
wa ccm Mwigulu Nchemba kumshawishi yeye
kuacha kugombea na kudai kuwa atapewa
ukuu wa wilaya akijitoa kwenye
kinyanganiro hicho kwa kupitia chama cha chadema.
"mimi nipigiwa simu tarehe Juni 12 saa tatu
asubui na mwigulu akitaka kuongea na mimi kwa madai kuwa ametumwa na rais
kuniuliza nitakacho ili niache kugombea udiwani kupitia chadema lakini
alivyokuja kwangu nilimwambia sitaki na meseji za ushaidi ninazo na mbali na
ivo nilitoa taarifa polisi kutokana na
swala hilo kwani nilivyomwambia sitaki alinijibu kuwa ccm ndo imekamata dola
naiwapo nitafikiria vizuri ni mpigie simu lakini adi leo sijawasiliana
nae"alisema Mpinga
Pia mpinga alikiri picha iliyopo kwenye mitandao
ni ya kwake akiwa na mwigulu nyumbani kwake lakini alishangazwa maelezo
yaliyowekwa na picha hiyo kuwa amejitoa na ajui muda aliyopigwa picha hiyo .
"nilikuwa namueshimu sana nchemba kama
mbunge wangu kwakuwa tumetoka kijiji kimoja lakini kwa ushenzi huu aliofanya
sitomuheshimu daima "alisema mpinga
Alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kujitokeza
kupiga kura kwa wingi kwani yeye
ajajitoa kugombea nafasi ya udiwani
kwani anawapenda wananchi wake.