MIRAA YAZUA MJADALA MZITO KATIKA BUNGE LA KENYA




Mjadala mkali umeibuka katika bunge la Kenya kuwa Mmea wa Miraa umesambaratisha maisha ya jamii, hivyo basi unapaswa kuorodheshwa kama Mihadarati mingine.

Bunge la Kenya sasa limelazimika kuteua kamati ya wabunge 30 kuchunguza manufaa au madhara yanayotokana na utafunaji wa miraa, kufuatia madai kuwa imevunja ndoa nyingi.


Mamlaka inayohusika na mikakati ya kupambana na  dawa za kulevya nchini Kenya -NACADA inaongoza kampeni ya kutaka Miraa (khat) ipigwe marufuku, wakisema ni mihadarati.


Jamii kutoka maeneo yanayopanda mmea huo kwa wingi, mfano jamii ya Meru katika mkoa wa Mashariki inasema kufanya hivyo ni kuwanyima kipato.


Wanalinganisha pato kutokana na Miraa na mapato ya jamii inayotegema mifugo kama ng'ombe, na sasa wabunge kutoka Meru wametetea zaidi kilimo cha Miraa.


Biashara ya miraa imesheheni katika miji yote nchini Kenya, na kuuzwa kwa wingi kwa watu wenye asili ya Kisomali Kaskazini Mashariki mwa Kenya na hata Somalia.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia