Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya, amelowa mvua ya
matusi baada ya kumfananisha mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
na aliyekuwa mwanamuziki mkubwa duniani, marehemu Michael Jackson.
Wikiendi iliyopita, Uwoya aliandika kwenye ukurasa wake katika mtandao
wa Instagram kuwa msanii huyo anayefanya vizuri katika Bongo Fleva ndiye
staa atakayemrithi mkali huyo wa Pop, maandishi ambayo yalizua matusi
hayo ya nguoni.
Baadhi ya mashabiki wa mastaa hao walitoa maoni kuwa jambo hilo ni sawa
na kufananisha vitu ambavyo havina uwiano hasa ukizingatia Michael
Jackson alishafariki dunia Juni 25, 2009.
“Sasa hiyo ni akili gani ya ki…(tusi) kumfananisha mtu aliyeko hai na
marehemu?” alihoji Mishish, mmoja wa mashabiki wa Uwoya katika mtandao
wa Facebook baada ya ishu hiyo kuwa gumzo mitandaoni.
“Kweli wewe Irene (Uwoya) ni …(tusi) au kwa sababu Diamond amesha…(tusi)
ndiyo maana unamsifia kiasi hicho,” aliandika shabiki mwingine kwenye
Twitter na kupisha wengine kuendelea kumporomoshea Uwoya matusi ya
nguoni.