Serekali
imetakiwa kusaidia kukuza utalii ulioko katika hifadhi za taifa
zilizoko katika ukanda waMagharibi, mikoa ya Mwanza, Kigoma na Rukwa kwa
kuwashirikisha mabalozi wa Tanzania waliko katika nchi Burundi na
kongo .
Hayo
yameelezwa na muhifadhi mkuu wa hifadhi ya Gombe iliyopo ndani ya ziwa
Tanganyika mkoani Kigoma Noelia Myonga wakati akiongea na waandishi wa
habari waliotembelea katika hifadhi hiyo.
Alisema kuwa iwapo serekali ita shirikiana na Tanapa kuunganisha balozi mbalimbali za nchi itasaidia kukuza utalii hapa nchini.
Alibainisa
kuwa katika miaka ya nyuma utalii uliokuwepo juu kabla ya kuvunjika
kwa amani kwa nchi za jirani ikiwemo Kongo na Burundi .
‘’nasema
hivyo kwa kuwa ukiangalia utalii uliopo katika nchi hizi unakaribia
kufanana na wanchini kwetu kwani ukiangalia katika nchi hizi kuna
wanyama ambao nao pia wapo huku ukiangalia mnyama aina ya Sokwe na
Gorila kwani wanyama hawa pia wanapatikana katika nchi hizi’’alisema
Mnyonga.
Alifafanua
kuwa pia serekali inatakiwa kuchukua hatua za makusudi za kuhifadhi
maeneo yaliyosalia ya makazi ya sokwe wapatao 1870 walioko nje ya mipaka
ya hifadhi .
Aliongeza
kuwa sokwe ni mnayama adimu sana anayepatikana katika baadhi ya mbuga
zilizopo hapa nchini hivyo serekali inatakiwa kujitaidi kushirikiana nao
ili kuweza kuwalinda sokwe hawa waliobaki ambao ni vivutio sana kwa
watalii wa ndani na wanje kwani tabia zake n maumbile yake yanakaribiana
na binadamu wa kawaida.
Mnyonga
alisema kuwa anapenda kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea
mbuga zao ili kujionea vivutio vilivyopo katika mbuga izo ambazo
zinavutia wangeni mbalimbai kutoka nje ya nchi.
Katika
hifadhi hii ya Gombe kuna vivutio vingi ikiwemo wanyama pori mbalimbali
kama vile sokwe mtu ,pia kuna maporomoko ya maji ambayo yanavutia mbali
na maporomoko kuna samaki wa aina mbalimbali wanaopatikana katika ziwa
Tanganyika pamoja na michezo ya maji ya aina tofauti tofauti.
HAKIKA INAPENDEZA SANA KUONA UTALII WA NDANI UNAENDELEZWA NA KILA MMOJA WETU KUONA VIVUTIO VYA UTALII KAMA ULIVYOFANYA WEWE DADA KUTEMBELEA GOMBE.INAPENDEZA KWELI NA UMETUELIMISHA
ReplyDelete