DIWANI WA CHADEMA AOMBA KURA KUPITIA SERA ZA CHAMA CHA MAPINDUZI





DIWANI mmoja wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyekuwa anagombea umakamu mwenyekiti wa halmashauri ya Geita, aliomba kura kwa kunadi sera za Chama cha Mapinduzi(CCM), imefahamika. Diwani huyo, Dioniz Bugali wa Kata ya Kamhanga, vilevile alimteua Diwani wa CCM kuhesabu kura zake.

Bugali alifanya kituko hicho mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Geita kwenye mkutano wa nne wa baraza la madiwani kwa mwaka wa fedha 2012/2013.


Katika uchaguzi huo wa makamu mwenyekiti wa halmashauri, mgombea wa wa CCM alikuwa Masoud Kimondo ambaye ni diwani wa kata ya Kaseme na kwa Chadema alikuwa yeyé, Bugali.

“Nimesimama hapa kuomba kura…kabla ya kuomba kura naomba niseme neno…nafasi hii ya makamu mwenyekiti wa halmashauri sikuwa naitaka isipokuwa nimelazimishwa na chama changu(CHADEMA)kugombea.

“Nachotaka kusema hapa ni kwamba nikishindwa sitakata rufaa.

“Ninampongeza sana mgombea mwenzangu wa CCM,mimi hapa pamoja na kuwa ni diwani wa Chadema na ninagombea nafasi hii kupitia chadema,lakini bado ni katibu mwenezi wa CCM kwenye kata yangu ya Kamhanga…nipeni kura zenu,”alijinadi Dionizi baada ya kupewa nafasi kuomba kura.

Kauli hiyo ilisababisha madiwani wa CCM kulipuka kwakicheko wakidai Bugali ni mwenzao na wengine wakiitambia Chadema kwa kusema, “Haloohalooooooooooooooo … Chadema mmesikiaaaa…hiyo ndiyo CCM…Spidi 120…Chadema hamna chenu Kamhanga huyo ni mwenzetu.”

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia