MAGAVANA WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA NCHI JIRANI WAKUTANA ARUSHA
Magavana
kutoka nchi za Afrika Mashariki na nchi majirani zao wamekutana jijini hapa
katika mkutano wao wa 13 pamoja na mengine kujadili mtangamano wa kuwa na sarafu
moja ya bara la Afrika kwa kuanzia na kuwa na mtangamano wa sarafu za kikanda.
Akizungumza
kwenye mkutano huo Gavana wa Tanzania Beno Ndulu alisema kuwa kuna chama cha mkutano
huu ujulikanao kama (CENTRAL BANK OF AFRICA SUMMIT) na kuwa mkutano huo ni wa
13 unaowakutanisha magavana na manaibu gavana kutoka kwenye wanachama wa chama
hicho.
Akazitaja
nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuwa ni
nchi za jumuiya ya Afrika mashariki na majirani zao nchi za congo drc,Ethiopia,
Sudan, Komoro,Mauritius,na Ghana mada kuu ya mkutano huo ikiwa ni kujenga
mtangamano wa sarafu ya pamoja kwa kuanzia na ukanda na baadae Afrika nzima.
Gavana Ndulu
alisema kuwa baada ya mawazo ya wakuu wa nchi wanachama wa AU kupitisha
maadhimio yao ya kutaka kuwa na sarafu za pamoja hivyo wao kama wadau wa sekta
ya fedha wanakutana kujadili mtangamano huo.
“Tunajiangalia
tutafikaje huko na je tumejiandaaje kufika huko hili ndio lengo la kukutana
hapa leo kwani timu hii ndiyo inadhamana ya kutufikisha huko”alisema ndulu
Mkutano huo
wa siku tatu unaowashirikisha wadau wa fedha kutoka kwenye nchi za afrika ulinza tangia juzi na kufunguliwa leo jijini
hapa na Gavana Ndulu
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia