HUYU NDO MWANAMKE HATARI AMBAYE ALITAKA KUMUUWA MUME WAKE ILI APATE MALI

MWANAMKE anayedaiwa kupanga njama za
kumuua mumewe wa ndoa na mtoto wamumewe, jana amefikishwa katika
Mahakama ya Wilaya Arumeru, iliopo Sekei, akiwa na mtuhumiwa mwingine wa
mauaji hayo.
Watuhumiwa hao ni Janeth Jackson (32),mkazi wa Moshono jijini Arusha
na Novatus Elias, walifikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha /Arumeru, Devotha Kamuzora na
kusomewa makosa mawili ya kula njama ya kutaka kumwua Simon Jackson
ambaye ndiye mume wa Janeth.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali,Edna Kasala alidai mahakamani hapo
kuwa, washitakiwa wote wawili, walitenda kosa la pili ya kula njama na
kutaka mumuua Desderi Sabas, ambaye ni mtoto wa nje wa mume huyo
anayeishi Bukoba mkoani Kagera.

Washitakiwa wote hawakutakiwa kujibu lolote mahakamani hapo, kwa
sababu Mahakama hiyo kisheria haina mamlaka ya kusikiliza kesi za
mauaji.
sababu Mahakama hiyo kisheria haina mamlaka ya kusikiliza kesi za
mauaji.
Mwendesha Mashitaka huyo wa serikali iliiomba mahakama kuwanyima
dhamana, watuhumiwa kwa sababu watuhumiwa wengine wawili katika kesi
hiyo bado wanatafutwa na hivyo kuwapa dhamana, kunaweza kuharibu
upelelezi ambao bado haujakamilika na washitakiwa hao wakatokomea
kusikojulikana.

Alisema kutokana na uzito wa tuhuma hizo, maombi hayo ya kuwanyima
dhamana watuhumiwa yameambatana na hati ya kiapo ya Mkuu wa Upelelezi
wa Makosa ya Jinai mkoani Arusha, akisisitiza kutowapa dhamana, licha
ya makosa hayo kuwa na dhamana.
dhamana watuhumiwa yameambatana na hati ya kiapo ya Mkuu wa Upelelezi
wa Makosa ya Jinai mkoani Arusha, akisisitiza kutowapa dhamana, licha
ya makosa hayo kuwa na dhamana.
“Mheshimiwa tunafahamu kwamba dhamana ni haki ya kikatiba ya kila
mtu,lakini kutokanana mazingira ya kesi hii kuwa magumu tunaomba
dhamana isitolewe, ili kuwatafuta watuhumiwa wengine wa kesi hii, na
hawa wasikimbie pia,’alisema MwendaMashitaka huyo.
mtu,lakini kutokanana mazingira ya kesi hii kuwa magumu tunaomba
dhamana isitolewe, ili kuwatafuta watuhumiwa wengine wa kesi hii, na
hawa wasikimbie pia,’alisema MwendaMashitaka huyo.
Kwa upande wake,Wakili wa Utetezi,Fidelis Peter alipinga maombi hayo
na kutaka mahakama itoe dhamana kwa washtakiwa, kwa sababu ni haki yao
ya kikatiba na kuwa hilo lilikuwa kosa lao la kwanza.
na kutaka mahakama itoe dhamana kwa washtakiwa, kwa sababu ni haki yao
ya kikatiba na kuwa hilo lilikuwa kosa lao la kwanza.
Alitoa sababu nyingine ya kupinga maombi ya upande wa mashitaka kwamba
sababu kuwa watuhumiwa wanaweza kuvuruga upepelezi akiachiwa, kuwa si
za msingi kwa ni watu wanaoaminika katika jamii.
sababu kuwa watuhumiwa wanaweza kuvuruga upepelezi akiachiwa, kuwa si
za msingi kwa ni watu wanaoaminika katika jamii.
“Mheshimiwa sababu za kuwanyima dhamana watuhumiwa hazina uzito wowote
pia mshitakiwa wa kwanza(Janeth) ana mtoto wa miezi sita na tangu
akamatwe alhamisi iliyopita hajamwona wala kumnyonyesha mwanaye hivyo
anastahili kupewa dhamana,”alisema Wakili Peter.
pia mshitakiwa wa kwanza(Janeth) ana mtoto wa miezi sita na tangu
akamatwe alhamisi iliyopita hajamwona wala kumnyonyesha mwanaye hivyo
anastahili kupewa dhamana,”alisema Wakili Peter.
Hata hivyo,baada ya kusikiliza maombi ya pande zote mbili. Hakimu
Kamuzora alikubaliana na maombi ya upande wa mashitaka na kuamuru
watuhumiwa warejeshwe ndani, hadi Agosti 5,mwaka huu,kesi hiyo
itakapotajwa tena.
Kamuzora alikubaliana na maombi ya upande wa mashitaka na kuamuru
watuhumiwa warejeshwe ndani, hadi Agosti 5,mwaka huu,kesi hiyo
itakapotajwa tena.
“Kutokana na uzito wa kesi hii, nakubaliana na hati ya kiapo ya Mkuu
wa Upelelezi ya kutowapa dhamana hadi hapo itakapobidi kufanya hivyo,
hivyo naomba mshitakiwa awe chini ya ulinzi,”alisema kamuora.
wa Upelelezi ya kutowapa dhamana hadi hapo itakapobidi kufanya hivyo,
hivyo naomba mshitakiwa awe chini ya ulinzi,”alisema kamuora.
Katika kesi hiyo iliyovuta hisia watu wengi jijini hapa,inadaiwa kuwa
Janeth alitaka kumwua mumewe ambaye ni mfanyabiashara ya madini
Ya tanzanite na mwanaye wa kiume ili arithi mali na utajiri alionao
mfanyabiashara huyo.
Janeth alitaka kumwua mumewe ambaye ni mfanyabiashara ya madini
Ya tanzanite na mwanaye wa kiume ili arithi mali na utajiri alionao
mfanyabiashara huyo.
Akiwa amejifunika uso muda wote alipokuwa mahakamani, Janeth
alionekana kuwa na mawazo mengi na macho mekundu kwa sababu ya kulia
baada ya njama hizo kugonga mwamba
alionekana kuwa na mawazo mengi na macho mekundu kwa sababu ya kulia
baada ya njama hizo kugonga mwamba
Hata hivyo nje ya Mahakama hiyo, habari za uhakika zilizopatikana
kutoka ndani ya familia hiyo, zimedai mshitakiwa huyo ana watoto
wawili ambao, mmoja ana miaka mitatu na mdogo ana miezi tisa na siyo sita kama alivyodai Wakili wa utetezi.
kutoka ndani ya familia hiyo, zimedai mshitakiwa huyo ana watoto
wawili ambao, mmoja ana miaka mitatu na mdogo ana miezi tisa na siyo sita kama alivyodai Wakili wa utetezi.
TAARIFA YA AWALI YA POLISI
JESHI la Polisi jijini hapa
limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja kati ya wawili waliyedaiwa
kuagizwa na Janeth Jackson kufanya mauaji ya mume wake ambae ni
Mfanyabiashara wa madini jijini hapa Jackson Kaijage pamoja na mtoto
wake wa kiume aliyezaa na mfanyabiashara huyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Kamanda wa Polisi wa jiji la Arusha, Liberatus Sabas, mtuhumiwa huyo
Novatus Elias Mrisha(35) alikamatwa na makachero wa jeshi hilo katika
mji wa Bukoba Mkoani Kagera akiwa katika hatua za mwisho za kutekeleza
mauaji hayo huku mtuhumiwa mwingine akitoroka.
Kamanda Sabas alisema kuwa baada ya
jeshi hilo la polisi kupata taarifa ya uwepo wa mpango wa mauaji hayo,
Julai 17 mwaka huu jeshi hilo lilituma makachero wake Bukoba kufuatilia
wauaji hao na kuwanasa.
Alisema makachero hao walifika Julai 18
mwaka huu na ilipotimu saa 4.00 usiku wauaji wakiwa katika harakati za
mwisho za kutekeleza mauaji kwa mtoto huyo wa kiume wa Jackson anayeishi
mjini humo walifanikiwa kumnasa mtuhumiwa mmoja aliyetajwa kwa jina la
Novatus Elias Mrisha (35).
“ Julai 18 mwaka huu saa 4.00 usiku
kikosi cha askari waliotumwa kutoka Arusha kwa kushirikiana na askari
Polisi Mkoani Kagera waliweza kumkamata mtuhumiwa mmojawapo kati ya
watuhumiwa wawili waliokuwa wamekwenda Bukoba kutekeleza mpango wa
mauaji ambapo mtuhumiwa Novatus mkazi wa moshono alikamatwa na mtuhumiwa
mwingine alifanikiwa kutoroka,”alisema Sabas.
Kamanda Sabas alisema kuwa mpango huo
wa mauaji ulipangwa kufanyika katika miji ya Bukoba kwa wauaji kumuua
mtoto wa mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 12 pamoja na ndugu
zake kadhaa na baadae kumalizia mpango huo wa mauaji kwa kumuua mume
wake Jackson Kaijage
maarufu kwa jina la ‘Jackson Manjuruu’ jijini Arusha.
maarufu kwa jina la ‘Jackson Manjuruu’ jijini Arusha.
Kamanda Sabas alisema baada ya
mtuhumiwa huyo kukamatwa na kuhojiwa alikiri kuhusishwa katika mpango
huo wa mauaji na kumtaja mke wa mfanyabiashara huyo kuwa ndiye
aliyewatuma kwenda kutekeleza mpango huo.
“Mke wa mfanyabiashara huyo aitwaye
Janeth Jackson (32), mkazi wa Moshono amekamatwa na anaendelea kuhojiwa,
watuhumiwa wote hao wawili watafikishwa mahakamani pindi upelelezi
utakapokamilika,”alisema Kamanda Sabas.
Kwa mujibu wa taarifa za awali zilidai
kuwa Janeth Jackson alipanga kumuua mumewe huyo kwa lengo la kurithi
mali walizokuwa nazo ikiwa ni pamoja na kuwaua mtoto wake na ndugu zake
wa karibu .
Wakati huo huo, Kamanda Sabas alisema
kwa jeshi hilo limekamata dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa
kilo 50 zilizokuwa zikisafirishwa na gari aina ya Nissan Mingroad namba
za usajili
T904 BSJ kutokea eneo la Unga limited kuingia katikati ya mji.
T904 BSJ kutokea eneo la Unga limited kuingia katikati ya mji.
Sabas alisema kuwa jeshi hilo lilipata
taarifa ya kubebwa mirungi ndani ya gari hilo na kuweka mtego ili
kuwanasa watuhumiwa lakini hata hivyo walifanikiwa kukamata dawa hizo
pekee kufuatia watuhumiwa waliokuwa wakiendesha gari hilo kulitelekeza
gari na kukimbia kusikojulikana.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia