SOMA HABARI SAHIHI DHIDI YA UVUMI KUHUSU WANAFUNZI WANAOENDELEA KULAZIMIKA KUJAZA TENA TAARIFA ZAO ZA MIKOPO YA ELIMU YA JUU

2704heslbKumekuwa na uvumi kwamba mtandao wa uombaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (OLAS) ulikuwa na hitilafu ya kiufundi na hivyo Wanafunzi wanaondelea na masomo ambao walikuwa tayari wameshahakiki taarifa zao wanapaswa kurejea kujaza upya ama kuhakiki iwapo taarifa zao zipo mtandaoni.
Bodi inatumia fursa hii kuwajulisha Wanafunzi husika, Vyuo vya Elimu ya Juu na Umma kwa ujumla kuwa taarifa za Wanafunzi hao zilizopokelewa ziko salama na hawapaswi kujaza tena na hivyo taarifa hizo za uvumi zipuuzwe.
Aidha Bodi inasisitiza  kwamba kesho tarehe 31 Julai, 2013 ni mwisho wa kupokea maombi ya mikopo ya waombaji wote wanaotarajia kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2013/2014 na wale wanaoendelea na masomo na kwamba hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.
Bodi inawapa nafasi ya mwisho waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao hawajaomba mikopo kwa njia ya mtandao, kuhakikisha wanatumia muda uliobaki kukamilisha taratibu zote za maombi kupitia anuani ifuatayo: http://olas.heslb.go.tz au kupitia tovuti: www.heslb.go.tz
Tangazo hili limetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia