Ngoma Africa Band aka FFU na
Mzimu wao muziki !
Bado unasumbua ughaibuni
Hakuna mashaka yeyote unapoutaja
muziki wa Tanzania katika Nyanja za kimataifa
Jina la Ngoma Africa band
maarufu pia kama “FFU Ughabuni”
inayoongozwa na
Mwanamuziki Kamanda Ras Makunja
wa FFU mwenye kukaanga mbuyu na wa
Kuwachia wenye meno kutafuna.
Kamanda Ras Makunja na kikosi
chake hicho Ngoma Africa band yenye maskani yake
Nchini Ujerumani,Ughaibuni ndio wanazidi kuwatia
wazimu washabiki wa muziki
Barani ulaya kwa kuitangaza
miziki ya Tanzania na kiafrika kwa kasi kubwa barani ulaya.
Bendi hiyo maarufu iliyoanzishwa mwaka 1993 na kiongozi wake
Ebrahim Makunja
Almaarufu Kamanda Ras
Makunja,imeweza kufanikiwa kuwapo katika medani ya muziki
Na kuweza kukonga nyoyo za
washabiki tangu ilivyoanzishwa,pamoja na mafanikio hayo
Ambayo sio kitu rahisi kuyafikia
kwa bendi za kiafrika barani ulaya,lakini kamanda
Ras Makunja na mzimu wake huo
Ngoma Africa band inaonekana kuwa ni hekalu
La ajabu!
Watafiti na tahasisi mbali mbali
za kimataifa za mambo ya itifaki katika medani ya muziki
Zimeelezea bendi hiyo kuwa na
washabiki au wapenzi wapatao milioni hamsini
(Milioni 50) kila kona duniani
kote, na kuifananisha bendi hiyo kuwa sawa na
Na muzimu mkubwa wenye mvuto na
mtandao wa mamilioni ya watu!
Watafiti wanashangazwa sana sana
kuona kuwa bendi hiyo maarufu ya kiafrika barani ulaya
Imekuwa na mvuto mkubwa kwa
washabiki,hadi sasa watafiti hawajagundua siri inayoifanya
Bendi hiyo kuwavuta washabiki kwa wingi!
Tunapozungumzia umaarufu na ustadi
wa Ngoma Africa Band ni sawa na kuzungumzia Moto
Mkali wa nyikani Usiozimika ! na
washabiki wake wapo tayari katika kila hali kuutetea mzimu wao
„Ngoma Africa Band“ ukipenda
FFU.
Ngoma
Africa band na Ushindi wa International Diaspora Award 2012
Juhudi za harakati za bendi ya
Ngoma Africa zimevuna matunda makubwa licha ya kuwanasa mamilioni
Ya washabiki wa kimataifa bendi
hiyo imeweza kuchagulia kuwa bendi bendi bora katika maonyesho mengi ya kimataifa yakiwemo maonyesho ya
“Expo 2000 Hannover” Germany na “Pacific World Music Festival
2000,Honolulu,Hawai.
Mwaka huu 2012 Kiongozi wa bendi
hiyo Kamanda Ras Makunja alitunikiwa tuzo ya kimataifa ya (IDA) International Diaspora Award,kwa niaba ya
bendi yake mjini Tubingen,Germany.
Ngoma Africa band inatajwa kuwa
ndio bendi ya kwanza ya kigeni barani ulaya kupewa tuzo hiyo ya kimataifa
,kutokana juhudi za bendi hiyo za
kuutangaza muziki na utamaduni kiafrika.
Kutokana na taarifa za tahasisi
ya Africa-activ Organizatation yenye makao yake Reutlingen, Ujerumani
zinailezea bendi hiyo kuwa ni urimbo mkali
unaowanasa mamilioni ya washabiki mara moja na mamilioni ya washabiki wapo taabani kwa mapenzi na mzimu huo wa
muziki Ngoma Africa band. Siri iliyiomo ndani ya bendi hakuna anayejua !! Labda mwenyewe Ras Makunja.
Wataalamu mbali mbali wa sosholojia na sekolojia ya maswala ya kijamii
wanaizungumzia bendi ya Ngoma Africa kuwa ni jinamizi lenye nguvu
kubwa za ajabu,jinamizi ambalo limetumia muziki wake kuwateka washabiki barani
Ulaya ! haijulikani nini siri ya
mvuto huo ! Jinamizi hili la “Bongo Dansi” ! pia limewapa wakati mgumu bendi
nyingi sana zinazo shea majukwaa katika
maonyesho ya kimataifa.
Ngoma Africa band ukipenda waiite
FFU ni bendi inayomilikiwa na washabiki na wapenzi wa bendi hiyo ambao wapo kila kona duniani,na
mafanikio haya ni mafanikio ya kujivunia watanzania.
Ngoma Africa Band imeweza
kuutawanya muziki wake katika vituo mbali mbali vya redio vya kitaifa na
kimataifa,
Zikiwemo redio za afrika
mashariki na ughaibuni,pia nyimbo hizo zinasikika katika mtandao au tuvoti ya
bendi hiyo