Mwenyekiti wa Klabu ya Simba akihutubia katika mkutano mkuu wa wanchama
kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterrbay Dar es Salaam leo.
Rage (katikati) akisindikizwa na baadhi ya askari kanzu kutoka kwenye mkutano huo
Mtoto Alhaji Samwel (11), mwanachama wa Klabu ya Simba kadi namba 696,
kutoka Ujiji Kigoma, akihojiwa na waandishi wa habari baada ya
kuhudhuria mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika Bwalo la Maofisa wa
Polisi Oysterbay, Dar es Salaam. Mtoto huyo alisema kuwa aliuwahi
mkutano huo kwa kusafiri kutoka Kigoma hadi Dar es Salaam baada ya
'kuzamia' kwenye treni (Reli ya Kati) bila kulipa nauli.
Wanachama wakihakikiwa kabla kuingia kwenye mkutano.
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Aden Rage (kushoto) akimkabidhi
mwanachama Hamis Kilomoni, nyaraka za mikataba ya mali za klabu hiyo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Aden Rage akisalimiana na wanachama wa
klabu hiyo baada ya mkutano mkuu wa klabu hiyo kumalizika kwenye Bwalo
la Maofisa wa Polisi Oysterbay, Dar es Salaam
Baadhi ya wanachama wa Simba wakishangilia baada ya mkutano huo kumalizika.
Baadhi ya wanachama wakiwa nje baada ya kumalizika mkutano huo