Wakazi wa kata nne za jimbo
la Arusha mjini leo(jana)wamepiga kura kwenye uchaguzi mdogo wa marudio baada
ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)kuwafukuza madiwani wake kutoka
kata za Elerai,Kaloleni,Kimandolu na Themi hali iliyopekea kuitishwa kwa
uchaguzi huu mdogo.
Miongoni mwa kata hizo ya
Themi uchaguzi umeendelea kwa amani licha ya kasoro mbali mbali zilizojitokea
ikiwemo ya watu kutokuta majina yao
kwenye ubao wa majina hali liyoleta sintofahamu kwa wakazi wa kata hiyo wakiwemo
wagombea kuhoji.
Akihoji suala la utata wa
kutokuwepo kwa majina ya wapiga kura akiwemo yeye mgombea wa CUF Lobora Ndarpoi
alisema kuwa ameenda sehemu aliyojiandikisha lakini hakukuta jina lake lakini
baada ya maelekezo ameweza kupata haki hiyo.
Ndarpoi alisema kuwa hali
kama hii itawafanya wananchi kutopiga kura na kupoteza haki yao ya kikatiba
huku akiwataka wakazi wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kutomia
haki yao ya kidemokrasia.
Akizungumza kwa upande
mwingine Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Themi Bi Eveta Mboya alisema
kuwa majina ya wapiga kura yalibandikwa takribani siku 30 na kuwa wananchi
walishindwa kuja kuhakiki.
Eveta alisema kuwa usumbufu kama huu ni
wakujitakia kwani kama ungeweza kuja kuhakiki hapa unajua upo kituo gani hili
ni tatizo na kuwataka wakazi wa kata hizo na watanzania kwa ujumla wake kujenga
mazoea ya kuhakiki majina yao kabla ya siku ya kupiga kura kukwepa usumbufu
kama huo.
“uhakiki ni jambo la muhimu
ili kukwepa usumbufu wa kutoona jina siku ya kupiga kura kumbe jina lipo kwenye
kituo chengine kama huyu hapa jina lipo Engira shule ya msingi yeye kaja
Zahanati kama angehakiki usumbfu kama huu
asingeupata”alisema Eveta.
Katika hali nyingine Gazeti
hili liliwashuhudia baadhi ya vijana wakiwaelekeza wenzao kumpigia kura mgombea
mmoja wa chama kimmoja ili aweze kupita katika uchaguzi huo
Hali ya uchaguzi katika kata
hizi inaonekana kuwa ya amani huku askari wakionekana kulinda amani hali
inayoufanya jiji kuwa kataka hali ya utulivu na Amani wananchi wengi wamekuwa
wakiendelea na shughuli zao za mwishi wa wiki.
Katika hali nyingine huko
kwenye kata ya Kimandolu kumeonekana hali ya sintofahamu baada ya vijana
waliokuwa wakipita wakiwa kwenye gari kukamatwa kwa kujaza gari na kupelekwa
kwenye kituo cha polisi.
Akizungumzia hilo kamanda wa polisi
mkoani hapa Liberatus Sabas alisema kuwa hao wahausiani na suala la uchaguzi
bali wamekamatwa kwa sheria za Trafiki kwa kuzidi abiria kwenye gari badala ya
abiria wanaotakiwa.