Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akipokea ua mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Sir Seretse Khama jijini Gaberone nchini Botswana kutoka
kwa binti Jessica Kissasi, anayesoma darasa la pili, Baobab
International School t arehe 29.7.2013.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Bwana Christopher Castle,Mkuu wa
Idara ya HIV and Health Education kutoka Makao Makuu ya Shirika la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yaliyoko Paris nchini Ufaransa
wakati Mama Salma alipowasiri kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir
Seretse Khama huko Botswana tarehe 29.7.2013.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akipewa maelezo mafupi na Dr. Patricia
Machawira, Mshauri Mkuu wa HIV and AIDS wa Nchi za Mashariki na Kusini
mwa Afrika muda mfipi kabla ya kuanza kwa mkutano wa “High Level
Group-Action on comprehensive sexuality education and health services
for adolescents and young people in Eastern and Southern Africa “
unaofanyika Gaberone nchini Botswana tarehe 30-31.7.2013.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa High Level Group wakisikiliza hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Mama Salma Kikwete
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akihutubia wajumbe wa mkutano wa sikuk mbili wa
“High Level Group” kutoka Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika
unaofanyika katika hoteli ya Lansmore Masa Square jijini Gaberone nchini
Botswana.
Baadhi
ya wajumbe kutoka Tanzania ( kulia kwenda kushoto) Dr. Kadija Mwamtemi,
Mwanahamisi Kitogo, Mshauri wa Rais kuhusu masuala ya huduma za jamii,
Ndugu Daud Nassib, Katibu wa WAMA foundation na Balozi wa Tanzania
nchini Botswana mwenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini Mheshimiwa
Radhia Msuya Mtengeti wakisikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi
iliyokuwa ikitolewa na Mama Salma tarehe 30.7.2013.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma
Kikwete akipongezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki
Mheshimiwa Jesca Eriyo baada ya kufungua mkutano wa “High Level Group”
huko Gaberone nchini Botswana terehe 30.7.2013.
Na Anna Nkinda- Gaborone, Botswana
Imeelezwa
kwamba ndoa za utotoni ni moja ya sababu inayowafanya watoto wa kike
kukatiza masomo yao huku asilimia 24 ya watoto hao wenye umri wa kati ya
miaka 15 hadi 18 wakiolewa katika nchi zilizopo kanda ya Mashariki na
Kusini mwa Afrika.
Kutokana
na umri wao watoto hao walitakiwa kuwa wanafunzi wa shule za Sekondari
na siyo kuishi na wanaume hivyo basi jitihada za pamoja zinatakiwa ili
kuhakikisha kuwa sheria na sera za kumlinda mtoto wa kike na kumjengea
mazingira salama ya kuishi zinatungwa.
Hayo
yamesemwa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na
wajumbe waliohudhulia mkutano wa kamati maalum ya viongozi
wanaoshughulikia huduma na elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka nchi
za Jumuia ya Afrika ya Mashariki (EAC) na Jumuia ya Ushirikiano wa
Maendeleo ya Kikanda kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika
katika Hoteli ya Lansmore Masa Square iliyopo mjini Gabarone nchini
Botswana.
Mama
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) alisema kuwa mkutano huo unafanyika kipindi ambacho jitihada
kubwa zinafanywa na nchi wanachama wa EAC na SADC ili kuhakikisha kuwa
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na mimba za utotoni zinapungua.
“Taarifa
ya Kanda inaonyesha kuwa Ugonjwa wa Ukimwi ni changamoto kwa vijana
wetu kwani kati ya maaambukizi mapya 620,000 yanatokea kila mwaka kuna
vijana wadogo wenye umri wa miaka 15hadi 24 kati ya hao asilimia 60% ni
wasichana hii inamaana kuwa kwa saa moja wasichana 31 na wavulana 21
wanapata maambukizi”, alisema Mama Kikwete.
Alisema
ili kukabiliana na tatizo hilo jamii inatakiwa kuhakikisha kuwa kuwa
mtoto wa kike anapata elimu ingawa idadi ya watoto wa kike ni kubwa
katika elimu ya msingi lakini wakifika elimu ya sekondari idadi yao
inapungua.
Mama
Kikwete alisema, “Ingawa kuna jamii zingine ni mwiko kwa wazazi kuongea
na watoto wao kuhusu afya ya uzazi lakini watoto hawa wanatakiwa
kufahamu afya ya uzazi na mabadiliko ya miili yao ili waweze kujikinga
na ugonjwa wa Ukimwi na mimba za utotoni”.
Alisema
nchini Tanzania kupitia Taasisi ya WAMA kuna kampeni isemayo mtoto wa
mwenzio ni wako mkinge dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi ambayo inaihamasisha
jamii kuwalinda watoto pia taasisi hiyo inafadhili elimu ya sekondari
kwa watoto ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi.
WAMA
imejenga mabweni ya wasichana katika shule za Sekondari, kutoa vifaa vya
maabara,huduma ya maji safi na kuhamasisha watoto wa kike kusoma masomo
ya sayansi pia kupitia klabu mbalimbali za wanafunzi mashuleni wametoa
elimu ya uzazi na jinsia ili vijana waweze kujilinda na maambukizi ya
HIV na kujikinga na mimba za utotoni.
Akifungua
mkutano huo Prof. Alaphia Wright kutoka UNESCO alisema mambo
watakayoyajadili yatapelekwa katika Serikali za nchi husika ili ziweze
kuongeza msukumo wa kisera na kibajeti na kuhakikisha kuwa wanatatua
changamoto za afya na uzazi zinazowahusu vijana.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia